Mkuu wa majeshi wa Korea Kaskazini ameondelewa madarakani, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo.
Ri Yong-Ho alipewa wadhifa huo miaka miwili iliyopita, kabla ya kifo cha kiongozi wa zamani wa Korea Kaskazini Kim Jong-il.Kuondolewa kwake mamlakani kunaangaliwa kama ishara ya mwelekeo wa utawala wa mwanawe kiongozi huyo wa zamani Kim Jong ill .
Shirika la Habari la serikali lilisema Bwana Ri amevuliwa madaraka yote ya kijeshi na kisiasa.
Mbali na kuwa mkuu wa Jeshi, naibu mwenyekiti wa tume Kuu ya jijeshi, yeye pia alishikilia vyeo kadhaa vikuu katika chama kinachotawala cha Workers Party.
Katika taarifa fupi chama hicho kilisema kiliamua kumwachisha madaraka yote Bwana Ri Yong kwa sababu ya ugonjwa.
Hata hivyo chama hicho hakikutoa taarifa zingine lakini ni wachache wanaamini kuwa ametimuliwa vyeo hivyo vyote kwa sababu ya maradhi pekee.
Bwana Ri alikabidhiwa madara ya Mkuu wa majeshi miaka mitatu iliyopita.
Alionekana mara nyingi karibu na kiongozi wa zamani, Kim Jong Il, na alidhaniwa kuwa angalikuwa kiungo muhimu katika kumkabidhi madaraka mwana wa kiongozi huyo, Kim Jong-un.
Kim-Jong-un, ambaye ametawala sasa kwa miezi sita, anaaminika kuwa na umri chini ya miaka 30.
Lakini Kim Jong-un anadhaniwa kuwa huenda akaanzisha mabadiliko kwa sababu uongozi wake unaoonekana kuwa bila ukakamavu wa baba yake.
No comments:
Post a Comment