Saturday, July 7, 2012

Mshindi katika uchaguzi wa Mexico atangazwa

Enrique Pena Nieto ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais nchini Mexico, baada ya kukamilika kwa zoezi la kuhesabu upya kura zilizopigwa.
 Pena Nieto aligombea kwa chama cha PRI kilichowahi kushikilia madaraka chini ya utawala wa kiimla  hadi kilipoondoka madarakani miaka 12 iliyopita.

 Baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 99 ya kura, Piena alionekana kujishindia asilimia 38 ya kura zote.


Mgombea cha chama cha mrengo wa kushoto Andres Manuel Lopez Obrador alikuwa katika nafasi ya pili, akiwa na asilimia 31. Zaidi ya nusu ya kura zilihesabiwa tena kutokana na hofu ya kufanyika kwa udanganyifu.  

No comments:

Post a Comment