Watu wamewasha mishumaa usiku wa kuamkia
Jumamosi(21.07)wakiwakumbuka wahanga wa mauaji mjini Colorado nchini
Marekani,katika utambulisho wa filamu ya Batman,ambapo watu12 wameuwawa
na wengine 60 wamejeruhiwa.
Mtu huyo ambaye alijifunika uso wake, akiwa amevalia mavazi meusi, kwa jina la James Holmes, mwenye umri wa miaka 24, aliingia katika jumba hilo la sinema , dakika 20 usiku wa manane wakati filamu ya "The Dark Knight Rises" , ilipokuwa ikioneshwa kwa mara ya kwanza, na kutupa mabomu ya kutoa machozi mawili na baadaye akafyatua risasi.
Baadaye alibadilisha idadi ya wahanga wa shambulio hilo, kutoka watu 70 hadi 71.
Watoto pia wauwawa
Hospitali ya mji huo inayowahudumia watoto imetoa idadi ya watoto waliouwawa kuwa ni sita, mdogo kabisa miongoni mwao akiwa na umri wa miaka sita. Wizara ya ulinzi ya Marekani , imesema kuwa takriban wanajeshi watu wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Karibu kila mtu alishambuliwa kwa risasi, amesema, na kuongeza kuwa , wachache wa watu ambao wamepata matibabu hospitalini hawakuwa na majeraha ya risasi, lakini walipata majeraha kutokana na mtafaruku.
Holmes ambaye anaripotiwa kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Colorado katika kitivo cha udaktari hadi mwezi uliopita, na hana rekodi ya uhalifu mbali ya kuonywa kwa kuendesha gari kwa kasi mwezi Oktoba 2011, kwa mujibu wa polisi.
Nyumba aliyokuwa akiishi karibu na mahala alipofanyia tukio hilo ilikutwa imetegwa mabomu. Polisi walitumia ngazi kujaribu kuingia katika nyumba hiyo kupitia madirishani.
Lakini Oates anasema kuwa operesheni hiyo imesitishwa hadi leo, Jumamosi.
Watu walioshuhudia wameeleza mtafaruku wa kutisha sawa na unaoonekana katika filamu ya Batman , ambapo watu wabaya wanatishia na kuwapa hofu watu wa mji wa Gotham.
No comments:
Post a Comment