|
wakati serikali ikisisitiza wananchi kwenda katika vituo kujiandikisha
ili kupata vitambulisha vya taifa wananchi katika halmashauri ya
manispaa ya Kinondoni kata ya Ubungo eneo la Msewe wamelalamikia
utaratibu Mbovu uliopo katika maeneo ya kujiandikisha ili kupata
vitambulisho vya Taifa. |
|
wakizungumza na blog ya habari na burudani leo hii katika shule ya
msingi ya ubungo msewe wananchi hao wamelalamikia utaratibu mbaya wa
uandikishaji kwa ajili ya kupata vitambulisho vya Taifa kwa malalamiko
kuwa utaratibu huo hauwadhiridhi kwa kuwa wamekuwa wakipoteza muda kwa
kupanga mistari kwa muda mrefu bila kupata huduma.
|
|
Wakiwa wamejipanga katika mstari kuelekea kwa karani wananchi hao walalamikia uchache wa makarani na wameomba serikali kuongeza makarani katika vituo vya kujiandikisha ili kuharakisha zoezi hilo la uandikishaji |
kwa upande wake karani ambaye blog hii iliweza kuongea bwana FLORIAN JUSTINE yeye amewataka wananchi wajitokeza kwenda kuona majina yao na pia kuhakikisha kuwa wanajiandikisha ili kuapata vitambulisha vya taifa zoezi ambalo litaisha katika eneo hilo july 30 mwaka 2012
karani Bwana Florian Justine kushoto Akiwa na Gasper sambweti (uncle G) wakati zoezi la kujiandikisha ili kupata vitambulisho vya taifa likiendelea
nami nilipata fursa ya kujiandikisha tayari kupata kitambulisho cha taifa
karani bwana Florian kulia akitoa maelezo jinsi ya kujiandikisha
hawa nao walikuwa wamejibanza na jua wakisubiri zamu yao kufika
No comments:
Post a Comment