Shirika la Save the Children,
limeonya kuwa ukosefu wa mvua ya kutosha na kuendelea kwa mzozo nchini
Somalia, kunatishia kusambaratisha mafanikio yaliyoafikiwa tangu mwaka
uliopita, wakati taifa hilo ilipokumbwa na baa la njaa.
Shirika hilo limesema ikiwa hali hiyo itaendelea, maisha ya maelfu ya watoto imo hatarini.
Shirika hilo la save the children, limesema idadi kubwa ya familia nchini Somalia, hawana uwezo wa kukabiliana na athari za ukame na kutoa wito wa kuongezwa kwa misaada zaidi ya dharura nchini Somalia.
Wakati huo huo, shirika hilo limetoa wito wa kubuniwa wa mikakati mipya ili kutambua na kusaidia taifa hilo kukabialana na athari za baa la njaa.
Mashirika kadhaa ya kutoa misaada ya kibinadam pia yametoa wito wa kuongezwa kwa misaada zaidi nchini Somalia, ambako maelfu ya watu waliangamia kutokana na baa la Njaa mwaka uliopita.
No comments:
Post a Comment