Kiongozi
wa jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, akiwa
amebeba maua, nakuzungukwa na amadaktari wenzake na wananchi wa kawaida,
alipowasili Jumapili Agosti 12, 2012, kwenye uwanja wa ndege wa
kiamataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwenye
matibabu Afrika Kusini. Alisema yuko fiti na anaweza kufanya shughuli
zozote atakazopewa kuanzia sasa.
hata hivyo baada ya Dk. Steven Ulimboka kuwasili uwanja wa ndege kulitokea mzozo baina ya wahandishi wa habari hasa wapiga picha mara baada ya ndugu wa Dk. Steven Ulimboka kuwanyima wahandishi hao kupiga lakini mzozo huo ulimaliza baada ya madaktari kuingilia kati na kulimaliza suala hilo.
Mara baaya ya Dk. Steven Ulimboka kuwasili alilakiwa na madaktari wenzake ,wananchi pamoja na wahandishi wa habari wengi wao wakiwa na shauku ya kumuona na pia kujua hali yake .
aidha Dk. Steven Ulimboka aliwashukuru madaktari wenzake pamoja na watanzania kwa ujumla kwa michango yao pamoja na sala zao ambazo hasa ndizo zilizomfanya kuwa hapo alipo.
Mara baada ya kusema hayo akiwa uwanjani hapo alipanda gari kuelekea nyumbani kwao kwani ni muda mrefu umepita .
blog hii inaungana na madakari pamoja na watanzania kumkaribisha Dk. Steven Ulimboka nyumbani kwani bado tunahitaji mchango wake katika kuokoa maisha ya watanzania .
No comments:
Post a Comment