Monday, August 13, 2012

Marekani na Misri kuilinda Sinai

Marekani na Misri kwa pamoja zinajaribu kutoa msaada mpya wa ulinzi katika eneo la Sinai kwa kuelezea  namna hali ilivyo mbaya kwenye eneo hilo.
Kwa mujibu wa gazeti la New York Times la Marekani, Jeshi la Misri limekuwa likiimarisha hali ya usalama katika eneo hilo kwa kufanya mashambulizi ya anga na ardhini tangu kutokea mauwaji ya walinzi 16 kwenye eneo la Sina lililopo mpakani baina ya Israel na nchi hiyo.
 Wanamgambo wa kiislamu waliofanya mashambulizi hayo wanaaminika kuwa na mahusiano na Army of Islam, kikundi kidogo cha wanamgambo wenye msimamo mkali wa kiislamu ambacho Misri imekuwa ikikituhumu kufanya mashambulio kadhaa nchini humo miaka iliyopita.

Taarifa za hivi punde zinasema kuwa vikosi vya serikali vya Misri vimewauwa wanamgambo watano katika mapambano kwenye eneo hilo hii leo.
 Shirika la Habari la Ujerumani, PDA linaarifu kuwa mshukiwa wa sita amejeruhiwa katika mapambano hayo yaliyofanyika kwenye eneo la al-Gura katikati ya Sinai. Vikosi hivyo pia vimefanikiwa kukamata mabomu na miripuko kwenye eneo la al -Kharbua, kaskazini mwa Sinai, baada ya kuwaweka kwenye ulinzi wanamgambo watatu.

No comments:

Post a Comment