Tanzania imesema kuwa wakala wa kusajili meli ulioko
Dubai ulizipa ruhusa ya kutumia bendera yake meli za
mafuta za Iran zipatazo 36 bila ya ridhaa au kibali cha
Tanzania.
Tanzania imesema kuwa kwa sasa iko kwenye mchakato wa kuziondolea usajili meli hizo baada ya kufanya uchunguzi juu ya wapi zinakotokea na kuthibitisha kuwa zinatokea Iran.
Tanzania ilianzisha uchunguzi mwezi uliopita kufuatia madai kwamba imezipa bendera mpya meli zinazosafirisha mafuta kutokea Iran na ikaziomba Marekani na Umoja wa Ulaya zisaidie kudhibitisha wapi zinatokea meli hizo zilizokuwa zinapepea bendera ya Tanzania.
Ripoti juu ya matokeo ya uchunguzi ilizungumzwa katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar ijumaa iliopita. Iran imewekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani, ikiwa ni shinikizo la kuifanya nchi hiyo iachane na mpango wake wa nyuklia unaoaminiwa na mataifa ya magharibi kuwa ni maandalizi ya kutengeneza silaha za atomiki.
Kitendo cha kutumia bendera za nchi nyingine kinaisadia Iran kufanya biashara yake ya mafuta bila kujulikana na Marekani pamoja na Umoja wa Ulaya.
Shirika la Mafuta la Iran limekuwa likibadili majina na bendera kwenye meli zake kuvikwepa vikwazo hivyo ambavyo vinaatihiri uchumi wake.

No comments:
Post a Comment