
Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji.
Raia
watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya
yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa
CHADEMA kuelekea kwenye mkutano.
Vurugu
zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video.
Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za
kuwasha toka Dar Es Salaam.
Tuombe
MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi
wamekusanyika kwa wingi hivi sasa. States captured by grand corruption
of the ruling party cronies for so many years’ resorts to bullets as a
way of stopping M4C through the ballot.
Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.
John John MNYIKA,
27 Agosti, 2012
No comments:
Post a Comment