Hii ndiyo taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa tarehe 22/8/2012 na wafanyakazi wa SUNRISE RADIO waliogoma kufanya kazi hadi mkurugenzi wa ufundi atakapo jiuzulu nafasi yake na madai ya wafanyakazi yatakapofanyiwa
kazi
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NDUGU
WANAHABARI SISI BAADHI YA WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO ARUSHA KUANZIA LEO
TAREHE 22/8/2012 TUMEAMUA KUGOMA KUENDELEA KUFANYA KAZI NA ASPIRE MEDIA COMPANY
LIMITED AMBAO NDIO WAMILIKI WA SUNRISE RADIO 94.8 FM ARUSHA BAADA YA KUSHINDWA
KUTIMIZIWA MAMBO KADHA WA KADHA
TULIYOKUWA TUNAYAHITAJI.
MGOMO
HUU ULIANZA KAMA MGOMO BARIDI MNAMO TAREHE 10/8/2012 BAADA YA SHEREHE ZA
WAKULIMA NANE NANE NA HII NI BAADA YA KUTOKEA TOFAUTI KATI YA MKURUGENZI WA
UFUNDI WA SUNRISE RADIO NDUGU DIONIS IDOWA SIKUTEGEMEA MOYO
DIONIS IDOWA SIKUTEGEMEA MOYO
|
NA KAMATI YA
SHEREHE ZA WAKULIMA NANE NANE MWAKA 2012 AMBAO NDIYO WALIOKUWA NA JUKUMU YA
KURUSHA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YAANI LIVE KUTOKA KATIKA VIWANJA VYA TASO
NANE NANE NJIRO.
NDUGU
WANAHABARI MGOMO HUU UMESABABISHWA PIA NA KUTOFANYIWA KAZI KWA MADAI YA
WAFANYAKAZI, WAFANYAKAZI TUMEKUA TUKIFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU KWANI:-
a)
TUNALIPWA MISHAHARA MIDOGO
ISIYOKIDHI MAHITAJI (MSHAHARA WA 100,000 NA WENGINE 170,000)
b)
KUFANYISHWA KAZI BILA KUWA NA
MIKATABA, TUKIDAI MIKATABA TUNAPIGWA TAREHE
c)
KUTOKATWA MAKATO KWENYE
MISHAHARA KWAAJILI YA PENSHENI
d)
BAADHI YA WAFANYAKAZI
KUFANYISHWA KAZI BILA KULIPWA
e)
HAKUNA OVERTIME PAYMENT
f)
WAFANYAKAZI KUTISHIWA KUFUKUZWA
MARA KWA MARA PALE WANAPODAI HAKI ZAO
g)
HAKUNA LIKIZO
h)
WAANDISHI WA HABARI WALIORIPOTI
LIVE YA UCHAGUZI WA ARUMERU MASHARIKI TAREHE 1/4/2012 KUTOLIPWA POSHO ZAO HADI
LEO NA WENGINE WALIDAI NA HATIMAYE WAKAFUKUZWA KAZI
i)
MISHAHARA WA WAFANYAKAZI
KUCHELEWESHWA KULIPWA KWANI UTAKUTA MSHAHARA WA MWEZI HUU TUNAWEZA KULIPWA
MWEZI UJAO KATIKATI AU MWISHONI
j)
MKURUGENZI WA UFUNDI KUTISHIA KUMFUKUZA KAZI MHASIBU KWA
MASLAHI YAKE BINAFSI
k)
WAFANYAKAZI WANAOFANYA VIPINDI
VYA USIKU KUTOPEWA USAFIRI WAKATI WA KWENDA NA KURUDI KITU AMBACHO
KINAMLAZIMISHA MTANGAZAJI KULALA STUDIO KWA LAZIMA
l)
GARI LA OFISI KUTOTUMIKA KWA
MAHITAJI YA OFISI BALI KWA MASLAHI YA MKURUGENZI WA UFUNDI
m)
MISHAHARA YA MWEZI JULY YA
BAADHI YA WAFANYAKAZI KUZUILIWA KUANZIA TAREHE 1/8/2012 HADI LEO HII TAREHE
22/8/2012 KWA SABABU ZISIZO ZA MSINGI
NDUGU
WANAHABARI, KWA MADAI HAYO HAPO JUU SISI WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO HATUPO
TAYARI KURUDI KAZINI MPAKA PALE MKURUGENZI WA UFUNDI NDUGU DIONIS IDOWA
SIKUTEGEMEA MOYO ATAKAPOJIUZULU NAFASI YAKE NA MADAI YA WAFANYAKAZI YATAKAPOKUA
YAMETATULIWA.
TUNAIPENDA
SANA SUNRISE RADIO BILA KUWASAHAU WASIKILIZAJI WETU PIA TUNAWAPENDA SANA ILA
TUMEONA NI VYEMA KUYAWEKA BAYANA HAYA YOTE ILI MTUELEWE NA PIA NI MAJIBU YA
BAADHI YA MASWALI MLIYOKUWA MNATUULIZA WASIKILIZAJI WETU WAPENDWA.
NDUGU
WANAHABARI WAFANYAKAZI WA SUNRISE RADIO WALIOGOMA KFANYA KAZI IDADI YAO NI KUMI
NA WAWILI (12) WAKIWEMO
a)
WATANGAZAJI 4
b)
MARIPOTA 2
c)
WATU WA MASOKO 3
d)
WAZALISHAJI WA VIPINDI 2 NA
e)
MHASIBU 1
WAFANYAKAZI
HAO WAMEGOMA KUTOKANA NA MADAI YAO HAPO JUU PAMOJA NA MADAI MENGINE MENGI
AMBAYO HAYAJAORODHESHWA
MAJINA
YA WAFANYAKAZI WALIOGOMA NI HAYA YAFUATAYO
1.
SEVERINUS MWIJAGE Jr –
MTANGAZAJI
2.
BEATRICE GERALD NANGAWE –
MTANGAZAJI
3.
EMMANUE MWAKALUKWA – MTANGAZAJI
4.
JALACK ALLY – MTANGAZAJI
5.
HAMIS ABTWAY (DJ HAAZU) –
MTANGAZAJI, MZALISHA VIPINDI NA DJ
6.
BERTHA ISMAIL – RIPOTA
7.
ONESMO LOY – RIPOTA
8.
JOSEPH AMANI – MZALISHAJI WA
VIPINDI
9.
ALLY CHARO – MENEJA WA MASOKO
10. RODGERS
I. NELSON – MHASIBU
11. WITNESS
RAYMOND – MASOKO
12. HAPPYNESS
ALPHONCE – MASOKO
ASANTENI
SANA KWA KUTUSIKILIZA
NAKALA
1.
MCT
2.
TCRA
3.
OFISI YA MKUU WA MKOA
No comments:
Post a Comment