Michezo ya Olimpiki ya London imesifiwa kuwa imezingatia sana mazingira - kushinda michezo yote iliyopita.
Mwenyekiti wa tume ya Olimpiki, Shaun McCarthy,alisema London imejipatia medali ya dhahabu kwa kuheshimu mazingira.
Michezo iliyopita ililaumiwa kwa uharibifu kwa sababu ya ubadhirifu mwingi uliotokea, lakini viwanja vya Olimpiki ya London, vilijengwa kwa nyenzo ambazo asilimia 25 zilikuwa zimeshawahi kutumika kabla.
Tume hiyo ilisifu mawasiliano baina ya viwanja mbalimbali vya Olimpiki, lakini ililalamika juu ya bidhaa za Olimpiki zinazouzwa, kama kweli zinazingatia mazingira.
Na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alitangaza Jumamosi, kuwa riadha na mashindano ya riadha yatakuwa sehemu ya ratiba mpya za shule.
Hatua hiyo inachukuliwa wakati kuna mjadala kuhusu mafunzo yaliyojitokeza kupitia Olimpiki kufanyika London; na inafuatia malalamiko dhidi ya serikali, kwa kuondoa nafasi za kufanya mazoezi shuleni.
No comments:
Post a Comment