Alisema
katika chama hicho kuna watu wengi wanaoweza kuwa wabunge wa jimbo hilo,
lakini yeye binafsi angependa Dk Slaa awe mbunge wa Arusha Mjini kwa
sababu Katibu Mkuu huyo wa Chadema akiwa bungeni ni moto wa kuotea
mbali.
Lema alisema: “Kuhusu ubunge wa Arusha sina hofu, atakuja Dk Slaa au mimi, ingawa sasa napenda aje Dk Slaa.”
Alisema
angefurahi kama Dk Slaa angekuwa mbunge wa jimbo hilo hasa katika
kipindi hiki cha kutafuta mabadiliko kumpokea wakati wa Uchaguzi Mkuu
wa mwaka 2015.
Lema alisema hivi sasa anafurahia mchango mkubwa anaoutoa katika chama chake akiwa nje ya Bunge.
“
Nahisi kutoa mchango mkubwa katika chama nikiwa nje ya Bunge kuliko
nilivyokuwa bungeni kwa sababu nimefanya shughuli nyingi zenye matokeo
chanya katika taifa hili,” alisema Lema.
Lema alienguliwa ubunge
mwaka huu na Mahakama ya Kuu Kanda ya Arusha kwa kilichoelezwa kuwa
alitumia lugha chafu katika kampeni za kuusaka ubunge huo mwaka 2010.
Kuchangia fedha za M4C
Lema
alieleza kuwa fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo zitatumika
kununulia helikopta, magari, pikipiki, baiskeli na matumizi mengine ya
Chadema kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa ukombozi kwa wananchi.
“Tusifanye
siasa ili kutafuta vyeo bali tulenge kuleta mabadiliko chanya katika
jamii iliyonyanyasika kwa muda mrefu. Nchi yetu ilipata uhuru, lakini
sasa tunahitaji mabadiliko yanayowakomboa wananchi kutoka kwenye
umasikini,” alisema Lema.
Kauli ya Mbowe
Akizungumza katika
harambee hiyo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa,
propaganda za ukabila, udini na rangi zinazoenezwa na CCM ni dhaifu na
zimeshindwa kuidhoofisha Chadema.
Alisema kuwa wananchi wamezishtukia propaganda hizo na kwamba, wananchi wengi wamehamasika kutaka mabadiliko.
Katika
harambee hiyo zaidi ya Sh270 milioni zilipatikana, kati ya hizo Sh250
milioni zikiwa ni ahadi na Sh20 milioni zikiwa ni fedha taslimu.
Kati
ya fedha hizo, Sh20 milioni zilichangwa na tawi la Chadema nchini
Marekani likiwa na majimbo yake Washington DC, Maryland na Virginia.
Watendaji wa Serikali
Kivutio
kikubwa kilikuwa kwa baadhi ya watendaji wa Serikali kuchangia katika
harambee hiyo na kutaka waitwe Wasamaria wema bila kutaja majina yao.
Mbowe
alisema: “Kwa kuwa wananchi wametuamini, tumeacha njia ya maandamano na
sasa tunataka kufika kila kata ya nchi hii ili kufikisha ujumbe wa
mabadiliko kwa wananchi. "
Alisema kuwa wamekubaliana baada ya
kumalizika kwa kikao cha Bunge wabunge wote wa Chadema watasambaa nchi
nzima kueneza Vuguvugu la Mabadiliko.
Mwenyekiti huyo wa Chadema
alisema kuwa mbali ya kufika kwenye kila kata chama hicho pia
kimejipanga kufikisha ujumbe huo katika nchi zote ambako kuna
Watanzania.
“ Hatuna mchezo sasa, tumejipanga kuchukua dola
ifikapo 2015, hawa CCM sasa ni kama wanaweweseka hawajui wanalolifanya,
tutawang’oa tu, ” alisema Mbowe.
Alisema kuwa chama hicho
kikifanikiwa kuchukua dola, kipaumbele kikubwa kitakuwa ni kuboresha
elimu ambayo ni sekta muhimu kwa maendeleo ya taifa.
“
Kipaumbele namba moja, mbili hadi tatu kitakuwa ni elimu. Tutawekeza
zaidi kwenye elimu ili kuwawezesha wananchi kuhimili changamoto za dunia
ya sasa hasa katika usimamizi wa rasilimali zao,” alisisitiza Mbowe.
Aliwahimiza
watu wanaokichangia chama hicho kwa kuficha majina yao kuacha hofu
akisema: “Jitokezeni hadharani, hamna sababu ya kuhofu kama kweli
mnahitaji mabadiliko. Tumepuuzwa, tumenyanyaswa na tumedhalilishwa kiasi
cha kutosha, sasa basi tuache woga.”
Alisema kuwa, CCM
imeshindwa kuwasikiliza madaktari, walimu na wafanyakazi wengine lakini
Chadema inaahidi kushughulikia matatizo ya makundi hayo.
Akizungumzia umuhimu wa harambee hiyo, Mbowe alisema mabadiliko yana
gharama zake na kwamba wadau ndiyo wanapaswa kuchangia chama hicho.
Mbowe aliomba kila mpenda mabadiliko kuchangia kwa kadri ya uwezo wake na kwamba fedha zake zitailetea mabadiliko nchi hii.
Vyeo
Akizungumzia
suala la nafasi za uongozi ndani ya chama hicho, Mbowe alisema kuwa,
huu si wakati wa kugawana vyeo wala kutangaza nafasi za kugombea bali
kukiimarisha chama ili kiweze kuwa na nguvu zaidi.
Naye Mwenyekiti
wa M4C, Mkoa wa Dar es Salaam, Alex Mayunga alisema harambee hiyo
ilikuwa na lengo la kukusanya Sh5 bilioni katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema
katika hafla ya jana walipanga kupata Sh500 milioni, lakini hazikutimia
kutokana na msongamano wa wananchi waliokuwa wakituma fedha kwa njia ya
simu za mkononi.
“Tunadhani hadi kesho (leo) kiasi hicho
kitatimia kwa sababu wananchi wengi wametuma fedha lakini bado
hazijatufikia,” alisema Mayunga.
Aliwataka wananchi kutuma fedha kwa kutumia njia ya simu za mkononi kwa sababu hiyo ndiyo njia rahisi. Mwisho
No comments:
Post a Comment