Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha, Claud Gwandu alisema Polisi imewazuia kufanya maandamano hayo kwa kisingizio cha ziara ya Rais Jakaya Kikwete.
Gwandu alisema maandamano yao ni ya amani na kwamba hayajapangwa kufika eneo ambalo Rais au mkutano wake utafanyika.“Tunakutana kujadiliana lakini polisi wamezuia wakitaka tupange siku nyingine kwa vile anasema askari wengi wa ulinzi watakuwa katika mkutano wa Rais na ziara yake,” alisema Gwandu.
Mikoa mingine
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsani alisema maandalizi katika klabu mbalimbali mikoani yamekamilika isipokuwa Ruvuma.
Alisema katika mkoa huo, UTPC imeagiza kusitishwa kwa maandamano hayo ili kupisha maandamano ya Chadema.
“Tumewaagiza waandishi kusitisha maandamano yao kupisha maandamano ya Chadema, kwani hatuwezi kuyachanganya na yale ya vyama vya siasa, hivyo wao wataandamana siku nyingine,” alisema.
Alisema tofauti na Mkoa wa Ruvuma, Mkoa wa Rukwa polisi ilizuia waandishi kuandamana kwa madai kwamba taarifa ilipaswa kutolewa saa 48 kabla ya kuandamana.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Shija Felician alisema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika.Alisema waandishi wa Zanzibar walikuwa katika maandalizi kwa ajili ya kufanikisha maandamano hayo.
Polisi wahaha
Katika hatua nyingine, askari wanne kati ya watano waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji hayo wameachiwa huru.
Habari zilizotufikia jana zimeeleza kuwa kuachiwa kwa askari hao kumekwenda sambamba na polisi kufanya jitihada za kumnusuru mtuhumiwa aliyebaki ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji.
Habari hizo zimeeleza kuwa, baada ya kukamatwa Jumatatu na kuhojiwa kwa siku tatu, askari hao waliachiwa na kuruhusiwa kurudi mikoani kwao.
“Walihojiwa na baadaye kuruhusiwa kurudi, lakini yule aliyeonekana kumlipua mwandishi huyo kwa bomu ambaye ameonekana kwenye vyombo mbalimbali vya habari anaendelea kushikiliwa,” kilidokeza chanzo cha habari ndani ya polisi.
habari kwa hisani ya http://alagwavideoproduction.blogspot.com/2012/09/maandamano-ya-waandishi-wa-habari.html?spref=fb
No comments:
Post a Comment