SAFARI,MALENGO YAKE KWENYE BURUDANI AZUNGUMZIA UHUSIANO WAKE KIMAPENZI
Kelvin Matandiko SAFARI
ni safari hata kama ni kwa Baiskel,Bodaboda,Gari au kwa miguu hiyo bado
itaitwa ni safari tu.siku zote mwanadamu anpoanza safari ya kuitafuta
ndoto yake itamlazimu ajitume kwa bidii ili aweze kufika.
Nikitaja
majina ya Watangazaji na Madj’s ambao ni kipenzi cha mashabiki wengi wa
muziki walioko kwenye chat kwa hapa nchini ni lazima utakutana na jina
‘Fetty’ hautalikosa katika ukurasa wowote wa burudani.
Binti huyu
ni shombeshombe wa kisomali aliyezaliwa Mkoani Shinyanga miaka fulani ya
themanini japo si mksukuma.Baadaye akaingia jiji la Dar es Salaam
ambapo alipata elimu yake yote ya sekondari.
‘Fetty’ anasema mwaka
2003 alivutia sana Babla Hassan wakati huo akitangaza kipindi cha ‘Hang
out’ saa sita mpaka saa nane mchana kituo hicho cha Clouds Fm.
“Kiukweli
alikuwa alinishawishi sana Safari ya kutimiza ndoto zangu za
utangazaji, sikuwa nimesomea kazi hii lakini niliamini kuwa nitaweza
mwaka wa 2004 nilienda ofisi za Clouds,niliomba kutangaza lakini haikuwa
rahisi baadaye nilianza kuingia studio kumsikiliza Babla
anavyotangaza”anasema Fet.
Kuanza kutangaza Fetty
anasema baada ya Babla kuacha kazi mwishoni mwa mwaka 2004 akitangaza
kipindi hicho alikabidhiwa kukiendesha ndani ya masaa 3,bila kuongea
hewani baadaye aliamua kuongea na Dj Nelly amfundishe kazi ya kuchezea
sahani za muziki,alionekana kufanya vizuri na ilipofika mwaka 2006 mambo
yakawa safi.
“Nikaanza kusikika kidogo kidogo kwenye kipindi cha
nyuki Dj’s ambapo kulikuwa na Jamaa sita na mtoto wa kike peke
yangu,kipindi hicho kilikuwa siku ya Jumamosi ndani ya masaa 3 na
nusu,ilipoanza julai 2006 tulianza kusikika mimi na ‘Muli B’
Anasema
baada ya kufanya vizuri alipewa ofa ya kwenda Uingereza kusoma kozi
fupi ya Utangazaji na alifanikiwa kurudi na wazo jipya la kipindi
alichokiita ‘soso fresh’ kilicho maanisha kila kitu sawa ambacho
kilifanya vizuri zaidi.
“Kipindi hicho nilikifanya kwa mwaka
mmoja baadaye mabosi wakaona nafanya vizuri wakanipa majaribio ya miezi
mitatu kipindi kikubwa cha ‘Top 20’ nikafanya vizuri,mashabiki
walinikubali sana baadaye wakaona ‘bongo fleva’ inapwaya ambayo
niliendelea nayo mpaka sasa.
Mafanikio yako “Nia
ya kuamua kufanya jambo fulani,Tamasha la Fiesta limenitoa sana
ukiachana na kazi ya utangazaji japo ndio kazi iliyonijengea kwa mambo
mengi,Tamasha la Fiesta ndio limefanya watu kunikubali zaidi,walikuwa
wanamsikia fet kwenye Radio kwa hiyo wanaposikia tamasha wanatamani
kumuona.nafasi ya Dj’s ni zaidi ya utangazaji kwangu.
Fetty
anasema kupitia kazi ya utangazaji na Dj imemletea mafanikio ya kuwa na
kampuni inayojulikana kwa jina la ‘fettylious’ inayohusika na matangazo
na kutengezesha nembo za tishet.kwa hiyo anasema maisha yake ni mazuri
kwa sababu anapata anachokita.
Ndoto zako Tukiachana
na tukio la kushangiliwa jumba la ‘Big Brother’ mwaka huu Fetty bado
anatamani siku moja aweze kusikika kwenye Vituo vya Radio za kimataifa
kama vile BBC na Aljazir,mbali na ndoto hizo anamshukuru Mungu kwa
nafasi aliyonayo kwa sasa kwani ametokea kuwa kipenzi cha watanzania
wengi wanaopenda Muziki.
“Tukio la Dodoma miaka 10 ya fiesta
nilishangaa watu walivyonipokea,walinitia moyo na kuamini kuwa
ninapendwa yaani maelfu walitamani kunishika hata mkono lakini
kilichosaidia ni askari.
Maisha yako na Jamii “Yako
poa sana ninaweza kujichanya na jamii yoyote hata tandale
naishi,sipendi mtu anayefanikiwa na kusahau alikotokea kwa mfano unaenda
Marekani miaka mitatu unarudi yes,no zinakuwa nyingi,unajifanya hujui
tena kiswahili.
Fetty anasema yeye anaweza kuongea lugha ya kisukuma vizuri tu japo sio lugha yake pamoja kuishi mjini kwa mda mrefu.
Chakula anachopenda “Hata
kama nipo usingizini ukiniamsha usiku wa manane kama nina njaa
nitakuomba Wali na Maharagwe ,ni chakula ambacho kwa kweli ninakipenda
sana kelvin.
Una mchumba “Da swali hilo kila
mtu huwa anapenda kuniuliza lakini huwa sipendi kueleza chochote juu ya
mahusiano yangu,wanaosema nina mtoto wa kigogo sio kweli maisha yangu
yasingekuwa haya pengine ningekuwa namiliki Benzi au Vog’,sitaki kuweka
wazi juu ya hilo.
Ila Fetty anapaza sauti mwanaume ambaye anaweza
kuishi nae akisema ni yule ambaye ataweza kutoa ushirikiano katika kazi
za ndani,anayemjali na kumthamini.
Ushauri kwa wanaopenda vya bure Fetty
anasema kila kitu ambacho kinapatikana kwa urahisi kina madhara hivyo
anawashauri wanawake wanaojiuza miili yao kwa kigezo cha umasikini
wafanye kazi,wajiunge kwenye makundi mbalimbali ya ujasiriamali.
“Uzuri
usitudanganye,sidhani kama ni safi kama ukiwa mzuri harafu maskini,bora
wanaume wakuone huwavutii lakini una pesa yako,inajenga heshima
kitaani,
“Wanawake tusipende kulia lia sana,nadhani msaada ambao
mwanamke anahitaji ni ukombozi wa kifikra.tusitumie kigezo cha jinsia
kutengeneza usawa hata kama mwanamke hana uwezo eti nafasi kwa sababu ya
kuweka usawa.
Changamoto ya ajira nchini “Watu
ni kweli wengi hawana kazi lakini isiwe kigezo cha kukaa na kubweteka
matokeo yake tunaingia kwenye makundi yasiyofaa,kazi ya uandishi wa
habari itapanuka sana mfumo wa digitali utakapoanza ila watanzania tuna
tatizo la ubunifu,wengi tuna ‘kopi na kupesti’
Taifa liweze kup[iga hatua ni lazima watu wawe wabunifu katika nyanja za kiuchumi,
Serikali yetu “Da
huwa sipendi sana kuzungumzia serikali lakini tatizo lililopo ni kwa
wabunge wetu,wengi hawana uwezo wa kupambanua hoja na tatizo ni
elimu,mbunge darasa la saba lazima katiba ijayo iweke kiwango cha elimu
ya wabunge, Wabunge mbumbumbu tuwapige chini,mbunge akiwa hivyo hawezi
kutunga hata sheria zenye manufaa kwetu.
Tanzania ya kesho “Natamani
sana kuona serikali inafanikiwa kuondoa changamoto ya foleni, yaani
msongamano wa magari imekuwa kero kubwa inakwamisha mambo mengi,ufisadi
unaongezeka wanakula pesa zetu kila kukicha,natamani kupata kiongozi
atakaye maliza kero hizi.
Habari makala hii ni kwa hisani ya gazeti la Mwananchi. |
No comments:
Post a Comment