Ryan wa Republican abainika kuomba msaada wa mafao
Masaa machache baada ya mdahalo wa wagombea wenza wa urais nchini Marekani, shirika la habari la Associated Press limechapicha ripoti inayoonesha kuwa Paul Ryan wa Republican aliomba msaada wa chakula, fedha za kujikimu na misaada mingine ya serikali nyuma ya pazia akiwa mjumbe wa Congress.
Shirika hilo la habari limehakiki nyaraka kadhaa zinazoonesha kwamba mgombea huyo mwenza wa Republican, aliunga mkono aina hiyo ya misaada ya serikali ambayo sasa yeye na mgombea wake wa urais, Mitt Romney, wanaipinga.
Barua zilizopatikana kupitia maombi ya umma, zinamuonesha Ryan akiomba fedha taslimu chini ya programu ya kufufua uchumi ya Rais Barack Obama au sheria ya huduma ya afya.
Katika kampeni zake, Ryan amekuwa akizipinga vikali programu zote mbili. Hata hivyo, msemaji wa Ryan amesema kwamba barua hizo zinaonesha tu kwamba Ryan alikuwa akitimiza wajibu wake wa kuwasaidia wapiga kura wake kukiuka urasimu wa serikali kuu.
No comments:
Post a Comment