Bomu la Vita vya Pili vya Dunia lagundulika Ujerumani
Zaidi ya watu 10,000 waliondolewa katika makaazi yao leo katika mji wa Potsdam hapa Ujerumani, baada ya kugundulika kwa bomu lenye uzito wa kilo 250 lililosalia katika Vita vya Pili vya Dunia.
Bomu hilo limepatikana katika sehemu ya kuegesha magari katika nyumba ya mkazi mmoja wa mji huo. Watu hao walirejea kwenye nyumba zao baada ya masaa kadhaa kupita na kukamilika kwa zoezi la kutegua bomu hilo katika hali ya usalama.
Ikiwa ni miaka takribani 70 baada ya kumalizika kwa vita vya pili vya dunia, bado kuna mabomu yanayokisiwa kufikia 10,000 katika ardhi ya Ujerumani ambayo hayajaripuka.
Mwezi Agosti, maafisa usalama mjini Munich walishindwa kutegua bomu lenye uzito wa kilo 250 na kulazimika kulipuliwa mahala. Mlipuko huo ulivunja madirisha ya nyumba kadhaa yaliyokaribu na lilipolipuliwa na pia kuzusha moto.
No comments:
Post a Comment