Kiongozi wa juu wa madhehebu ya Salafi, Sheikh Hisham al-Saedini na wapiganaji wawili wameuawa katika shambulio la anga usiku wa kuamkia leo huko Gaza, huku Israel ikiahidi leo kupambana vikali dhidi ya wapiganaji wa Jihadi.
Katika mashambulizi mawili ya kwanza ambayo yaliofanyika kaskazini mwa mji wa Jabaliya jana jioni, kikosi cha anga cha Israeli kiliwaua wapiganaji wa madhehebu ya Salafi, Sheikh Hisham al-Saedini na Fayek Abu Jazar, shambulio la pili kama hilo lililokuwa likiwalenga Waislamu wenye itikadi kali ndani ya wiki moja.
Saa chache baadae, ndege za kivita za Israeli ziliwalenga wapiganaji wawili wa kundi la PLPF kusini mwa mji wa Khan Yunis na kumuua mmoja wao Yasser Mohammad al-Atal na mwingine kujeruhiwa vibaya.
Akizungumza na baraza la mawaziri leo asubuhi, Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu amesema wapiganaji wa Jihadi wanaongeza majaribio yao ya kuwadhuru Waisraeli na ameonya kwamba jambo hilo halitavumiliwa.
No comments:
Post a Comment