Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (MB) leo ametangaza rasmi
matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne, maarifa-QT.
TAARIFA YA
MATOKEO YA MITIHANI YA MAARIFA (QT) NA KIDATO CHA NNE (CSEE)
ILIYOFANYIKA
OKTOBA 2012
1.0
UTANGULIZI
Mitihani ya
Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) kwa mwaka 2012 ilifanyika nchini
kote kuanzia tarehe 8-25 Oktoba 2012.
Napenda kuchukua nafasi hii kutangaza rasmi matokeo ya mitihani hiyo
kama ifuatavyo :
2.0
MTIHANI WA MAARIFA (QT)
2.1
Usajili na Mahudhurio
Katika Mtihani
wa Maarifa 2012 watahiniwa waliosajiliwa ni 21,310 ambapo wasichana
walikuwa ni 13,134 na wavulana ni 8,176.
Jumla ya watahiniwa 17,137 sawa na asilimia 80.42
ya waliosajiliwa wamefanya Mtihani.
2.2
Matokeo ya Mtihani wa
Maarifa (QT)
Watahiniwa 5,984
kati ya 17,137 waliofanya
mtihani wamefaulu Mtihani wa Maarifa (QT).
3.0
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2012
Jumla ya vituo 5,058 vilitumika
katika kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ambapo vituo 4,155 vilikuwa vya watahiniwa wa shule na vituo 903 vilikuwa ni vya watahiniwa wa kujitegemea.
3.1
Usajili na Mahudhurio ya Watahiniwa
(a)
Watahiniwa Wote
Jumla ya watahiniwa 480,036 walisajiliwa
kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2012 wakiwemo wasichana 217,583 sawa
na asilimia 45.33 na wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67.
Watahiniwa waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne 2012 ni 456,137
sawa na asilimia 95.44. Watahiniwa
21,820 sawa na asilimia 4.55 ya watahiniwa wote waliosajiliwa
hawakufanya mtihani.
(b)
Watahiniwa wa Shule
Watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni
411,230 wakiwemo wasichana 182,978
sawa na asilimia 44.50 na wavulana 228,252
sawa na asilimia 55.50. Watahiniwa wa shule waliofanya mtihani
walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57. Aidha, watahiniwa 14,090
sawa na asilimia 3.43 hawakufanya
mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, ugonjwa na vifo.
(c)
Watahiniwa wa Kujitegemea
Watahiniwa wa
kujitegemea waliosajiliwa walikuwa ni 68,806 wakiwemo wasichana 34,605
sawa na asilimia 50.29 na wavulana 34,201 sawa na asilimia 49.71.
Watahiniwa 61,001 wakiwemo wasichana 30,917 na wavulana 30,084 wamefanya mtihani wakati watahiniwa 7,730
sawa na asilimia 11.23 hawakufanya
mtihani.
4.0
MATOKEO YA
MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
(a)
Watahiniwa wa Shule
Jumla ya watahiniwa wa shule 126,847 kati ya
watahiniwa 397,136 waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne
2012 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni 46,161 na wavulana ni 80,686.
(b)
Watahiniwa wa
Kujitegemea
Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu
mtihani ni 16,112 kati ya
watahiniwa 61,001 waliofanya mtihani. Wasichana waliofaulu ni 6,751 na
wavulana ni 9,361.
5.0
UBORA WA
UFAULU KWA MADARAJA NA JINSI
Ubora wa ufaulu kwa
kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule unaonesha kuwa jumla
ya watahiniwa 23,520 wamefaulu katika madaraja I – III ambapo
kati yao wasichana ni 7,178 na wavulana ni 16,342.
Mchanganuo wa ufaulu kwa
kila Daraja kwa jinsi kwa Watahiniwa wa Shule mwaka 2012 ni kama ifuatavyo:
Idadi ya Wavulana
|
Idadi ya Wasichana
|
Jumla
|
|
I
|
1,073
|
568
|
1,641
|
II
|
4,456
|
1,997
|
6,453
|
III
|
10,813
|
4,613
|
15,426
|
I-III
|
16,342
|
7,178
|
23,520
|
IV
|
64,344
|
38,983
|
103,327
|
0
|
120,664
|
120,239
|
240,903
|
6.0
SHULE
ISHIRINI ZILIZOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU
ZAIDI
Ubora wa ufaulu wa shule umepangwa kwa kutumia kigezo cha “Grade
Point Average” (GPA) kuanzia A = 1 hadi F = 5. Shule zenye watahiniwa 40 na zaidi ziko 3,391. Shule ya kwanza hadi ya ishirini
zimeainishwa kwenye Jedwali lifuatalo :
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
ST. FRANCIS GIRLS
|
90
|
MBEYA
|
2
|
MARIAN BOYS S.S
|
75
|
PWANI
|
3
|
FEZA BOYS S.S
|
69
|
DAR ES SALAAM
|
4
|
MARIAN GIRLS S.S
|
88
|
PWANI
|
5
|
ROSMINI S S
|
78
|
TANGA
|
6
|
CANOSSA S.S
|
66
|
DAR ES SALAAM
|
7
|
JUDE MOSHONO S S
|
51
|
ARUSHA
|
8
|
ST. MARY’S MAZINDE JUU
|
83
|
TANGA
|
9
|
ANWARITE GIRLS S S
|
49
|
KILIMANJARO
|
10
|
KIFUNGILO GIRLS S S
|
86
|
TANGA
|
11
|
FEZA GIRLS
|
49
|
DAR ES SALAAM
|
12
|
KANDOTO SAYANSI GIRLS SS
|
124
|
KILIMANJARO
|
13
|
DON BOSCO SEMINARY SS
|
43
|
IRINGA
|
14
|
ST.JOSEPH MILLENIUM
|
133
|
DAR ES SALAAM
|
15
|
ST.JOSEPH’S ITERAMBOGO SS
|
64
|
KIGOMA
|
16
|
ST.JAMES SEMINARY SS
|
44
|
KILIMANJARO
|
17
|
MZUMBE SS
|
104
|
MOROGORO
|
18
|
KIBAHA SS
|
108
|
PWANI
|
19
|
NYEGEZI SEMINARY SS
|
68
|
MWANZA
|
20
|
TENGERU BOYS SS
|
76
|
ARUSHA
|
7.0
SHULE KUMI
AMBAZO HAZIKUFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KUNDI LA SHULE ZENYE WATAHINIWA 40 AU
ZAIDI
NAFASI
|
JINA LA SHULE
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
MKOA
|
1
|
MIBUYUNI S.S
|
40
|
LINDI
|
2
|
NDAME
S.S
|
41
|
UNGUJA
|
3
|
MAMNDIMKONGO S.S
|
63
|
PWANI
|
4
|
CHITEKETE S.S
|
57
|
MTWARA
|
5
|
MAENDELEO S.S
|
103
|
DAR ES SALAAM
|
6
|
KWAMNDOLWA S.S
|
89
|
TANGA
|
7
|
UNGULU S.S
|
62
|
MOROGORO
|
8
|
KIKALE S.S
|
60
|
PWANI
|
9
|
NKUMBA S.S
|
152
|
TANGA
|
10
|
TONGONI S.S
|
56
|
TANGA
|
8.0
TATHMINI YA
UFAULU WA WATAHINIWA WA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
8.1
Tathmini ya awali iliyofanyika kuhusu ufaulu wa watahiniwa katika shule
mbalimbali inaonesha kuwa shule zilizofanya vizuri zaidi ni zile ambazo zina
mahitaji yote ya msingi ikiwemo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya
kufundishia na kujifunzia. Aidha, shule
zenye ufaulu wa chini ni zile ambazo zina changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja
na:
(i)
Baadhi ya
shule za vijijini hazina kabisa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati na pia
zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo mengine;
(ii)
Kutokuwepo
kwa maabara kwa shule zenye mikondo ya sayansi na pia kutokuwepo kwa maktaba
kwa ajili ya kujisomea; na
(iii) Upungufu mkubwa wa vitabu vya
kiada na ziada. Katika baadhi ya shule uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi ni 1:10.
8.2
Mkakati wa
Serikali ni kuendelea kupunguza changamoto hizo kila mwaka ikiwa ni pamoja na
kufanya mambo yafuatayo:
(i)
Kuajiri
walimu kila mwaka ili kuondoa upungufu uliopo katika shule zetu. Mwaka 2011/2012
Serikali iliajiri walimu wa sekodari 13,246 na mwaka huu wa fedha 2012/2013
imeajiri walimu 12,973 ambao wamepangwa katika shule zenye
upungufu mkubwa wa walimu. Ajira ya walimu wapya mwaka huu umetuwezesha kuwa na
wastani wa walimu 2-3 kwa shule.
Hali hii itaendelea kuboreka kadri tunavyoendela kuajiri walimu.
(ii)
Kuboresha
miundombinu iliyoko katika shule zetu ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba za
walimu, madarasa na maabara. Mwaka 2012/2013 Serikali imepanga kuboresha
miundombinu katika shule 264 zilizopo katika mazingira magumu ikiwemo miundombinu
ya maabara na nyumba za walimu.
(iii)
Kuendelea
kutoa ruzuku ya Tsh 25,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka, ambapo asilimia 50
ya fedha hizo ni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia
ili kuziwezesha shule kununua vitabu pamoja na vifaa vingine muhimu kitaaluma.
(iv)
Wizara
kuendelea kuzishauri Halmashauri kuweka mgawanyo mzuri wa walimu waliopo baina
ya shule na shule.
(v)
Wizara
itaendelea kuimarisha Idara ya Ukaguzi wa Shule pamoja na kuwawezesha Waratibu
Elimu Kata na Wakuu wa Shule kufanya ukaguzi wa ndani katika Shule za Sekondari
zilizo katika maeneo yao.
9.0
MATOKEO YA MITIHANI YALIYOZUIWA
Baraza la Mitihani la
Tanzania limezuia kutoa matokeo ya:
(a)
Watahiniwa 28,582 wa Shule ambao hawajalipa ada ya Mtihani hadi watakapolipa ada
wanayodaiwa pamoja na faini; na ikiwa hawatalipa katika kipindi cha miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
(b)
Watahiniwa 65 wa kujitegemea na 71 waliofanya
Mtihani wa Maarifa (QT) mwaka 2012 bila ya kulipa ada ya Mtihani hadi
watakapolipa ada pamoja na faini. Ikiwa hawatalipa ada hiyo katika kipindi cha
miaka miwili (02) toka matokeo kutangazwa, matokeo yao yatafutwa.
10.0
MATOKEO YA MITIHANI
YALIYOFUTWA
10.1
Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Udanganyifu
Jumla ya watahiniwa 789 wamefutiwa matokeo yao yote ya mtihani kwa
mujibu wa kifungu Na.52(b) cha Kanuni za Mitihani baada ya kubainika
kuwa walifanya udanganyifu katika mitihani ya Oktoba 2012. Kati yao,
watahiniwa wa shule ni 624 na watahiniwa wa kujitegema ni 148 na
watahiniwa wa Mtihani wa Maarifa (QT) ni 17.
Aina ya udanganyifu uliobainika na idadi ya watahiniwa husika ni kama
ifuatavyo:
S/N
|
AINA YA UDANGANYIFU
|
IDADI YA WATAHINIWA
|
(i)
|
Watahiniwa kubainika kuwa na skripti zenye miandiko tofauti au kuwa na
miandiko tofauti katika skripti ya somo moja au zaidi ya moja.
|
04
|
(ii)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa
na ‘notes.’
|
170
|
(iii)
|
Watahiniwa kubainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu.
|
590
|
(iv)
|
Watu kukamatwa wakiwafanyia watahiniwa wengine mtihani
‘impersonation”.
|
04
|
(v)
|
Watahiniwa kukamatwa na simu ndani ya chumba cha mtihani.
|
06
|
(vi)
|
Watahiniwa kukamatwa na wasimamizi wakibadilisha karatasi za maswali
au skripti kwa lengo la kufanya udanganyifu.
|
15
|
JUMLA
|
789
|
10.2
Matokeo Yaliyofutwa Kwa Sababu ya Watahiniwa Kuandika
Matusi Katika Skripti Zao
(i)
Jumla ya watahiniwa 24 waliandika matusi kwenye skripti zao za masomo mbalimbali. Kitendo hicho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5(13) cha Kanuni za Mitihani
kinachosomeka:
“Written responses to any examination
question which carry words, drawings or pictures connected to sex or abusive
language in such a way that it becomes offensive shall consitute an examination
offence and a candidate who commits such an offence shall be punished by the
Council.”
Kutokana na kosa
hilo Baraza la Mitihani limefuta matokeo
yao yote kwa mujibu wa
Kifungu cha 6(2)(a) cha Kanuni za
Mitihani kinachosomeka:
“A candidate
found to have committed an examination offence shall - (a) have his examination
results nullified”
(ii)
Kitendo cha kuandika matusi kwenye karatasi za majibu (skripti)
kinaonesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Serikali haitaweza kuwavumilia hata
kidogo watahiniwa wa aina hiyo. Hivyo, Serikali itaangalia hatua zaidi za
kisheria za kuchukua dhidi ya watahiniwa wote walioandika matusi.
Kwa
mujibu wa kifungu Na. 6(2)(b) cha Kanuni za Mitihani, watahiniwa wote
waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani au kuandika matusi katika
skripti zao hawataruhusiwa kufanya mitihani inayoendeshwa na Baraza la Mitihani
la Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja
(01) kuanzia tarehe ya kutangazwa kwa matokeo.
11.0
KUANGALIA MATOKEO YA
MTIHANI WA CSEE na QT, 2012
(a)
Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT), 2012 yanapatikana katika tovuti zifuatazo:
·
www.udsm.edu.ac.tz, au
·
www.moe.go.tz
(b)
Matokeo yanaweza kupatikana pia kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwenda namba 15311.
Jinsi ya kutuma ujumbe andika:
MATOKEOXNAMBA YA KITUOXNAMBA YA MTAHINIWA
(Mfano : matokeoxS0101x0503)
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO
YA UFUNDI
No comments:
Post a Comment