Wednesday, April 24, 2013

CHAMA CHA MCHEZO WA VINYOYA JIJINI DAR ES SALAAM LAANDAA SHINDANO KUANZIA 26 APRIL -1 MAY


Nylon Shuttlecock

Chama cha  mpira wa vinyoya (badminton) jijini Dar es salaam limeanda mashindano ya  mchezo huo wa vinyoya   umeandaliwa baada ya  kikao cha kamati kilichokaa hivi karibuni, kilipanga mashindano ya mchezo huo kuzinduliwa Aprili 26, Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kumalizika siku ya Wafanyakazi duniani.


akieleza lengo la mashindano hayo  katibu wa  chama cha mpira wa vinyoya  amesema  mashindano yataamsha ari  kutimiza adhima ya kuimarisha mchezo huo pia  kurudisha heshima kwa jamii baada ya mchezo huo kusua sua kwa muda.

akiongea na waandishi wa habari katibu wa chama hicho Wilbard Kente  amesema kamati I ya utendaji ya muda ya Chama cha Mpira wa Vinyoya Tanzania (TBA), imeandaa mashindano maalumu yatakayoshirikisha timu za mkoa wa Dar es Salaam.

Katibu Kente amesema mchezo huo wa vinyoya uliifanya Tanzania kujulikana duniani miaka ya 1970, kutokana na kushiriki michezo ya kimataifa.

“Kamati yetu imedhamiria kufufua mchezo huu kwa kuandaa mashindano ya vilabu kadhaa vya jijini Dar es Salaam, ili kuinua mchezo huu,” alisema Kente.

Feather Shuttlecock
Kente alizitaja klabu hizo kuwa ni Badminton Institute, Khalsa spot club Upanga, Lohana, Shshikungi, Jensen, Dar es Salaam Institute, Aga Khan, Bhatia, Bhohora, Shnashel, Anadil Burhan na Sigh Community.

Aidha, aliziomba klabu hizo kujitayarisha, ikiwemo kujisajili ifikapo Aprili 25 mwaka huu na Aprili 26 hadi Mei Mosi kilele chake, ambacho wanatarajia Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, kuwa mgeni rasmi.

nae katibu msaidizi wa chama hicho cha mpira wa vinyoya TONY DESOUZA amewaomba vijana wa rika zote kujiunga na mchezo na kuepuka kukaa kwenye vikundi visivyo na maana .

mwisho kabisa katibu msaidizi aliweza kueleza hali ngumu inayowakabili ya upungufu wa pesa katika club yao  na kuomba  wale wote wanaopenda kufadhili mchezo wa vinyoya wanakaribiskwa  kwani milango iko wazi  na mwisho kabisa maewakaribisha wananchi kujitokeza kuangalia mchezo huo  wa kusisimua katika kipindi cha michuano hiyo  ambayo washindi watapata vikombe mbali mbali.


No comments:

Post a Comment