Wanafunzi wapatao 14 leo wamezawadiwa kompyuta mpakato /laptop
katika halfa ya chakula chamchana kilichoandaliwa kuadhimisha miaka 10 ya fao la Elimu iliyofanyika
katika ukumbi wa mwalimu Nyerere Dar es salaam.na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali kama waziri wa kazi na ajira mhe.Gaudensia Kabaka,Naibu waziri wa fedha mhe. Saada Mkuya Salum,Naibu waziri wa katiba na sheria mhe;Anjelina Kairuki,mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe.Said Mecky Sadiki,Naibu katibu mkuu was maendeleo ya jamii ,jinsia na watoto Bi. Anna Maembe,kamishna wa elimu profesa .Eustella Bhalalusesa mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa sekta ya hifadhi ya jamii ( SSRA) ,Ndugu Irene Isaka na wengine wengi.
Wanafunzi hao
walizawadiwa zawadi hizo na mgeni rasmi mama Salma kikwete,ambaye
amepongeza mfuko wa pensheni PPF kwa
kuanzia fao hilo kwani kwa mwaka jana
pekee waliweza kusomesha wanafunzi zaidi ya 1333 katika shule mbali mbali za
msingi na sekondari hapa nchini Tanzania bara na visiwani.
Watoto wanaofadhiliwa na mfuko wa pensheni
wa PPF ni watoto ambao wamepoteza mzazi
kati ya baba au mama na mwanachama awe ameshachangia mfuko kwa zaidi ya
miaka 3 au zaidi , na mwanafunzi atapata fursa ya kusomeshwa kwa kulipiwa karo
na mahitaji mengine kama sare za shule
vifaa( stationeries)usafiri, chakula kwa kuzingatia mshahara wa mzazi aliyekuwa mwanachama wa PPF na watoto wanasomeshwa kuanzia awali( chekechea ) hadi kidato cha nne na pia wasizidi watoto wanne..
Nae
mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa
PPF bwana Wiliam Erio ameelezea mafanikio makubwa ya shirika hilo tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1978 na kusema kuwa mapato ya shirika hilo yameongezeka
kila mwaka ,hii imewezesha thamani ya
mfuko kufikia shilingi trilioni moja nukta sifuri kenda (1.09)mwezi desemba
mwaka 2012.
Aidha mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya
mfuko wa pensheni wa PPF proffesa Adolf Faustine Mkenda katika hafla hiyo aliweza kuelezea changamoto
3 zinazokabila fao hilo la elimu kuwa ni
baaadhi ya shule kutotuma taarifa za mitihani za wanafunzi wanaosomeshwa na fao
hilo.
Changamoto nyingine inayokabili fao hilo ni
udhibitisho wa uhakika kuwa wanaosomeshwa ni wale wanaostaiki na sio watoto
wengine,na changamoto nyingine ni
waajiri kuchelewa kutuma taarifa za vifo vya wafanyakazi mara wanapofariki
hivyo wanafunzi hupata usumbufu wa kuchelewa kulipiwa karo hususan kifo
kinapotokea wakati wa mwanzo wa masomo hivyo huadhiri maendeleo ya mwanafunzi.
Ombi la mgeni rasmi kwa mfuko wa pensheni
wa PPF ni kuangalia kama hali itaruhusu waweze kuongeza ,kipindi cha kusomesha
kutoka kidato cha nne hadi kidato cha
sita ili kumuwezesha mwanafunzi kuweza
kufikia malengo ya kielimu kuliko kumsomesha mpaka kidato cha nne elimu amabyo
haitamruhusu kuendelea kusoma ,pia
amependekeza na kuomba hivyo akijua fika kuwa kama mwanafunzi atasomeshwa mpaka
kidato cha sita basi ataweza kuendelea na chuo kikuu kwa kuwa vyuo vikuu vinatoa mkopo kwa wanafunzi.
Mwisho mgeni rasmi mama salma kikwete
aliwaasa wanafunzi waliofanya vizuri na kuzawadiwa kompyuta mpakato kutumia kwa
matumizi sahihi na ya kielimu zaidi na sio kwa vitendo vya kuvunja maadili na
kupotosha maadili katika jamii.
No comments:
Post a Comment