Kampuni zinayofanya biashara ya utumaji wa fedhwa nchini Somalia kwa kushirikiana na Benki ya Barclays zimeiomba benki hiyo kutofunga akaunti zao kwani hatua hiyo itafanya maisha kuwa magumu kwa wanaotegemea huduma hiyo.
Wasomali wengi wamekuwa wakitegemea njia hiyo kupokea fedha kutoka kwa ndugu na jamaa wanaoishi nje kupitia huduma hiyo kutokana kukosekana kwa mfumo kamili wa kibenki nchini humo.
Benki ya Barclays inatarajia kufunga akaunti za kampuni hiyo mwezi ujao,imesema ina wasi wasi juu ya utumaji fedha haramu.
Mamilioni ya watu wanategemea pesa zinazotumwa kwa njia hiyo, ambazo utafiti wa hivi karibuni umesema kuwa pesa hizo zinafika dola bilioni laki tau na nusu kila mwaka.
No comments:
Post a Comment