Wednesday, June 19, 2013

TAN TRADE YATOA SEMINA KWA WASHIRIKI MBALI MBALI WA MAONYESHO YA 37 YA SABA SABA 2013

Washiriki mbali mbali kutoka katika mashirika na vyama mbali mbali vya ujasiriamali  kutoka nje na ndani ya Tanznia leo wamepatiwa semina yenye  mafunzo mbali mbali katika maandalizi ya  maonyesho ya 37 ya saba saba  yatakayoanza hivi karibuani  katika viwanya vya Mwalimu nyerere vilivyopo kilwa road jijini  Dar es salaam.

Akifungua semina hiyo  iliyofanyika leo mkurugenzi wa Tan Trade  bi Anna F.Bulando ameelezea maonyesha haya ya 37 kuwa yatakuwa maonyesho makubwa ya kimataifa na ya kipekee kufanyika jijini Dar es salaam ukilinganisha na maonyesho ya miaka mingine kwani maonyesho haya yatashirikisha nchi nyingi zaidi  kuliko miaka  yote.


Nchi zitakazoshirkia katika maonyesho ya mwaka huu  zimeongezeka kutoka nchi 11 zilizoshiriki mwaka jana na kuongezeka hadi kufikia nchi 32  ambazo zitashiriki katika maonyesho hayo mwaka huu.

mada zipatazo sita zimeweza kujadiliwa na kutolewa mafunzo kwa washiriki ili kuhakikisha kuwa wanafuata na kuzingatia  hatua hizo ambazo kama wakifuata na kuheshimu basi watapata mafanikio makubwa katika biashara zao na pia kuzidi kuwa vutia washiriki wengine ambao bado hawajaonyesha nia ya kushirikia maonyesho ya saba saba.

baadhi ya mada au masomo yaliyotelewa kati ya sita ni elimu juu ya wajibu wa kila mshiriki  kuhusu afya,usalama wa vyakula  na usafi wa mazingira uliotolewa  na afisa afya wa manispaa ya  Temeke bwana William muhemu.

aAmbapo alikazia zaidi kuhusu kila mshiriki kuhakikisha kuwa wakati wa maonyesho h ayo kila moja anakuwa msafi na kufuata kanuni za afya  ili kuhakikisha kuwa shughuli zote za  maonyesho ya 37 ya saba saba yanakwenda vizuri bila kutekea kwa maambuzi ya magonjwa ya mlipuko ambayo mara nyingi hutokea katika mikusanyiko mikubwa ya watu ambao hawafuati  sheria na taratibu za afya  pindi waendapo na watokapo katika maliwat na pia katika ulaji mbaya ambao mara nyingi  watu hujikuta wakilishwa kinyesi cha binadamu bila wao kujua  kutokana na kula katika magenge  ya watu wanaotoa huduma bila kuwa wasafi na hivyo kusabisha kulipuka kwa magongwa ya milipuko kama kipindu pindu.

  mada nyingine iliyopata wasaa wa kujadiliwa ni pamoja na mada ya  upakiaji  au auandaa na usafishaji wa bidhaa  ambao  uanatakiwa uwe na viwango madhubiti unaokubalika na mamlaka  ya  viwango Tanzania TBS kwa kuhakikisha kila mjasirialamali anafuata  njia sahihi za uandaa na usindikaji wa bidhaa yake katika  viwango vinavyokubalika na Tbs mada hiyo ilitolewa na  bi Mary Meela kutoka TBS.

Mada nyingine ni masoko ya ndani na nje  na  mfumo wa  ufuatiliaji  na masoko ya kimataifa  iliyotolewa na Bwana Pius Mikingoti  wa GS1  Tanzania, mada nyingine ni madaraja na viwabgo vya bidha  vinavyotengezwa na kusafirisha  au kuuzwa kwa mteja /mlaji au mtuamiaji  iliyotolewa na Bwana kiteka na  mada nyingine ni kuhusu kodi  ambayo mada hii imeandaliw ana kutolewa na bi. Rose Mahendeke  kutoka TRA.

No comments:

Post a Comment