Rais Jakaya
Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama
wakipokea saluti wakati nyimbo za Taifa zikipigwa ,wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa Marekani leo katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa
Julias Nyerere .
Nyuma yao
ni mama Salma Kikwete na mama Michelle
Obama pamoja na mkuu wa majeshi Davis Mamunyange pamoja na IGP Said Mwema .
Kushoto ni
mkuu wa itifaki Balozi Mohamed Maharage
na mkuu wa itifaki wa ikulu ya Marekani
( white House ) balozi capricia
Marshall..Ziara ya Rais Obama inatajwa
kuwa moja kati ya ziara za viongozi wan je zilifanikiwa sana,
ambapo pia maelfu ya Watanaznia waljitokeza kumlaki na kumuaga.
Rais Barack
Obama akiagama na mstahiki Meya wa jiji
la Dar es salaam huku Mstahiki Meya wa
Ilala pamojana Balozi wa Tanzania nchini Marekani mhe.Liberata Mulamula
wakisubiria zamu zao za kuagana na Rais wa Marekani.
|
HAOOO Rais Obama
na mkewe wakikwea pipa lao la Air Force One tayari kwa safari ya kurudi
nchini Marekani mara baada ya kumaliza ziara ya siku Mbili nchini TANZANIA.
Rais
kikwete na mama Salma Kikwete wakiagana
na wageni wao katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere leo .
|
Rais
Kikwete ,Mama Salma na Kikwete,Naibu
Waziri wa kilimo mhe Adam Malima
(kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ,balozi wa Marekani hapa nchini Mhe.Alfonso
lenhardt wakiwapungia mikono kuwaaga wageni wao ambao wamemaliza ziara yao ya siku mbili hapa nchini Tanzania
baada ya k ufika jana na kufika ikulu kisha
kuongea na Rais wa Tanzania Mhe.DKT
JAKAYA KIKWETE na baada ya hapo alipata fursa ya kuongea na waandishi
wahabari .
Pia Rais
Barack Obama alipata wasaa wa kuzindua
barabara iliyotambulika kama OCEAN ROAD hapo awali na Jana kubatizwa na kupewa
jina jipya la BARACK OBAMA DRIVE ,
Pia kwa
siku ya leo Rais Obama aliweza kutembelea kinu cha kufua umeme cha symbion kilichopo
Ubungo Tanesco karibu kabisa na
kituo maraarufu cha daladala cha Ubungo .
No comments:
Post a Comment