Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu
mabadiliko ya Tabianchi, Chanagamoto za Maendeleo na ukuaji wa Miji
Barani Afrika. Mkutano huo umefunguliwa leo Julai 24, 2013 Jijini
Arusha. (Picha zote na OMR)

Arusha.
Profesa Rwekaza Mukangara, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo. Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi. Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
Na Richard Mwangulube, Arusha
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea zawadi ya Jarida la Sayansi, kutoka kwa Mkurugenzi wa Sayansi
'Physical Sciences' (COSTECH), Profesa Clavery Tungaraza, baada ya
Makamu kufungua rasmi mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount
Meru, Jijini Arusha leo Julai 24, 2013.
Profesa Rwekaza Mukangara, akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais kufungua mkutano huo. Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya ufunguzi rasmi. Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi. Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi.
Na Richard Mwangulube, Arusha
MAKAMU
wa Rais, Dk. Mohamed Bilal amewataka watunga sera na watoa maamuzi
barani Afrika kupitia upya sera za mipango miji ili miji iweze
kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.
Akifungua
mkutano wa Kimataifa unaojadili changamoto zitokanazo na ukuaji kasi wa
miji, ongezeko la watu mijini na maendeleo pamoja na mabadiliko ya
tabia nchi jijini Arusha leo, Dk. Bilal alisema maafisa mipango miji
wanatakiwa kubuni mipango bora itakayowasaidia wakazi wa mijini
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa miaka ya hivi
karibuni yamekuwa ni changamoto kubwa.
“Kuna
haja kubadilisha mipango yetu ili miji iweze kuhimili ongezeko la watu
pamoja na mabadiliko ya tabia nchi,” alisema Bilal.
Alisema
kuwa asilimia 75 ya nishati inayotumika mijini na nje ya miji na pia
asilimia 80 ya taka ngumu inazalishwa mijini na miji hutoa zaidi ya
asilimia 60 ya hewa ya ukaa angani, hali ambayo huchangia kuongezeka kwa
hali ya ujoto duniani.
Makamu
wa Rais alisema katika miaka ya hivi karibuni bara la Afrika limekuwa
likishuhudia ukame na mafuriko ya mara kwa mara hali ambayo imekuwa
ikichangia ongezeko la umaskini na kushuka kwa uchumi katika nchi
nyingi.
“Hali
hii imekuwa ikiwaathiri sana watu maskini hususani wale wanaoishi
kwenye makazi duni, hivyo ipo haja kwa watunga sera na watoa maamuzi
kukaa chini na kubuni mikakati bora itakayosaidia kukabiliana na
mabadiliko hayo,” alisisitiza, na kuongeza: “Miji mingi Afrika inaweza
kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, kama nia
na mipango mizuri itaandaliwa.”
Alitaja
baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kuwa na miongozo na sheria
imara ambazo zitazuia watu kujenga kwenye mabondeni ambako kuna hatari
ya kukumbwa na mafuriko na maporomoko.
Bilal
ambaye ni mtaalamu wa masuala ya nyuklia alisisitiza umuhimu wa watu
kubadili tabia na kuacha mtindo wa kufanya mambo wa mazoea ili kupunguza
madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema
kuna haja pia kuwa na mipango ya pamoja ya kidunia itakayosaidia
kupunguza madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
Akiwasilisha
mada kwenye Mkutano huo, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha
Ardhi, Profesa Alphonse Kyessi alisema asilimia 70 ya wakazi wa Dar es
Salaam wanaishi kwenye maeneo yasiyopimwa hali inayowafanya wakazi hao
kukumbwa na maafa yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi.
“Hali hii ipo kwenye miji mingi barani Africa,” alisema Profesa Kyessi .
Alisema
idadi ya watu waishio mijini imekuwa ikiongezeka karibu kila mwaka
barani Africa. “Hivi sasa idadi hiyo imekuwa ikikua kwa asilimia 40 na
tafiti zinaonyesha kuwa kufikia mwaka 2050 idadi hiyo itakuwa kwa
asilimia 61.8.”
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala alisema
chuo chake kimeanzisha kituo maalum kwa ajili ya kufundisha wanafunzi
kuhusiana na masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema hatua hiyo inalenga kuongeza idadi ya wataalam kwenye eneo hilo nyeti .
Mkutano
huo wa siku tatu unaowakutanisha wataalam mbalimbali kwenye masuala ya
mabadiliko ya tabia nchi kutoka Afrika na kwingineko duniani umeandaliwa
Kituo cha Mabadiliko ya Tabia Nchi cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa
kushirikiana na Kamisheni ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Mamlaka
ya Hali ya Hewa (TMA), Chuo Kikuu cha Ardhi na Shirika la Marekani la
START Secretariat.
No comments:
Post a Comment