Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametunukiwa tuzo ya kimataifa ya jitihada za kuendeleza rasilimali watu katika taifa kwa mwaka 2012 na Taasisi ya Bright Entertainment Network (BEN) ya nchini Uingereza.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt.Fenella Mukangara wakati akitoa maelezo mafupi kuhusiana na tuzo ya Ben TV Diplomatic Awards-2012 aliyopewa dhamana na Taasisi ya Bright Entertainment Network (BEN) ya Uingereza ya kumkabidhi Mama Salma Kikwete Tuzo hiyo katika jitihada zake za kuendeleza rasilimali watu katika Taifa kwa mwaka 2012.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara akimkabidhi Tuzo ya Ben TV Diplomatic Awards-2012 Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ofisini kwake tarehe 19.8.2013. Tuzo hiyo ilitolewa kwa Mama Salma baada ya kuibuka mshindi miongoni mwa mataifa ya bara la Afrika, Caribean, Asia na Pacific kutokana na kazi za kuendeleza rasilimai watu hapa Tanzania.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba fupi ya kushukuru mara tu baada ya kupokea Tuzo kutoka kwa Taasisi ya Bright Entertainment Network ya Uingereza iliyokabidhiwa kwake na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara tarehe 19.8.2013.
Mwnyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo mara baada ya Waziri Mukangara kumkabidhi Tuzo hiyo
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment