Tuesday, August 27, 2013

REDD'S MISS ILALA ATOA MSAADA WA VITABU VYA SH. 300,000 SHULE YA MSINGI GULUKA KWALALA,UKONGA,DAR


Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel amkimkabidhi  vitabu mwanafunzi Charles Costantino ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya Shule ya Msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mollel alikabidhi vitabu 30 vyenye thamani ya sh. 300,000. Wanaoshuhudia ni Miss Ilala namba mbili Alice Issack (wa tatu kushoto), mshindi wa tatu Clara Bayo (wa pili kushoto) na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Rehema Mketo.
Malkia wa Redd's Miss Ilala 2013, Doris Mollel akiwa na wanafunzi baada ya kukabidhi msaada wa vitabu  30 vyenye thamani ya sh. 300,000 kwa Shule ya msingi Guluka Kwalala, Jimbo la Ukonga, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 Warembo wakifurahi pamoja na wanafunzi
 Mshindi namba tatu Clara Bayo akizungumza na mmoja wa wanafunzi.
 Mollel akimkabidhi zawadi shs. 5000 mwanafunzi aliyejibu swali walililoulizwa wanafunzi
  wakiwa katika piacha ya pamoja na wanafunzi pamoja na Mwalimu Mkuu
 Warembo wakiwa na mwalimu wa shule hiyo, Lugano Mwaikambo ambaye aliwahi shiriki Miss Morogoro mwaka 2000.
 Warembo wakicheza michezo mbalimbali na wanafunzi wa shule hiyo


Warembo wakicheza Nage na wanafunzi

No comments:

Post a Comment