Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akiwa katika picha Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark
Rutte,alipofika katika Ofisi ya Waziri huyo Nchini The Hague Uholanzi
akiwa katika ziara na Ujumbe aliofuatana nao.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark
Rutte,alipofika katika Ofisi ya Waziri huyo Nchini The Hague Uholanzi
akiwa katika ziara na Ujumbe aliofuatana nao,(kushoto) Waziri wa
Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akifuatana na Mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark
Rutte,baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri huyo
Nchini The Hague Uholanzi akiwa katika ziara ya Kiserikali na Ujumbe
aliofuatana nao.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akisalimiana na Bibi Regine Aalders,kutoka Wizara ya Afya nchini
Uholanzi,wakati alipotembelea katika Ofisi ya Kampuni ya Sakura Finatek
jana,ambayo inatengeneza Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa Binadamu,nje
ya Mji wa The Hague Nchini Uholanzi akiwa katika ziara ya Kiserikali.
Bibi
Regine Aalders,kutoka Wizara ya Afya nchini Uholanzi,alipokuwa
akiwasilisha mada wakati wa mkutano wa kampuni ya Sekura na Makampuni
mengine wakati walipokutana na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
nchini humo kwa ziara ya Kiserikali ambapo ziara hiyo itamalizika kesho.
Baadhi
mya Viongozi wa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wenyeji wao
Viongozi wa kampuni ya Sakura Finetek Europe,inayojishuhulisha na
Utengenezaji wa Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa Binadamu,iliyopo nje
ya Mji wa The Hague Nchini Uholanzi wakiwa mkutano wa kufikia kuongeza
kasi ya kutoa huduma bora za Kiafya katika ziara ya Kiserikali.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akitoa hutuba yake wakati wa mkutano na Kampuni ya Sakura Finetek
Europe, inatengeneza Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa Binadamu,wakati
alipotembelea katika Ofisi ya Kampuni hiyo jana,iliyopo nje ya Mji wa
The Hague Nchini Uholanzi,Rais akiwa katika ziara ya Kiserikali.
Baadhi
ya Viongozi na Maafisa wa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
wakiwa katika mkutano wa Ushirikiano na kampuni ya Sakura Finetek
Europe,katika hatua za makusudi katika kuongeza kasi ya utoaji wa Huduma
za Kiafya,walipokuwa katika ziaraya Kiserikali nchini Uholanzi.
Baadhi
ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika mkutano wa
Ushirikiano na kampuni ya Sakura Finetek Europe,katika hatua za
makusudi katika kuongeza kasi ya utoaji wa Huduma za Kiafya,walipokuwa
katika ziara ya Kiserikali nchini Uholanzi.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mtaaalamu wa matumizi ya Vifaa vya
maabara Robert Heijmen,alipotembelea mashine mbali mbali za uchunguzi
wakati wa mkutano na Kampuni ya Sakura Finetek Europe, inayotengeneza
Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa maradhi ya Binadamu, jana akiwa
katika ziara ya kiserikali nchini uholanzi.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,akipokea Cheki kutoka kwa Rais,pia Meneja Mkuu wa kamapuni ya
Sakura Finetek Europe, Chris Koeman,kwa ajili ya Uchunguzi wa Maradhi ya
binadamu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,wakati wa mkutano wa ushiriano
katika kukuza huduma na kampuni hiyo,na Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar,katika ziara Nchini Uholanzi.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na
ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kamapuni ya
Sakura Finetek ,baada ya mkutano uliofanyika jana baina ya kampuni na
Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ukiwa katika ziara Nchini Uholanzi. .[
Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
No comments:
Post a Comment