Makamu mwenyekiti wa UTPC Bi Jane Mihanji akitoa tamko la UTPC dhidi
ya Chadema kutaka kutumia kifo cha Mwangosi kisiasa.
Rais wa UTPC Bw Keneth Simbaya kushoto akimpongeza makamu wake Bi Jane Mihanjo kwa tamko zuri alilolitoa.
Akitoa
tamko kwa niaba ya bodi ya UTPC jana , Makamu wa Rais Jane Mihanji
wakati mkutano mkuu maalumu wa kupitisha marekebisho ya Katiba ya UTPC
uliyofanyika Mjini Dodoma kwa muda wa siku mbili.
Alisema kuwa Chama hicho kisitumie kifo cha mwandishi wa habari huyo kujinufaisha katika maslahi binafsi ya kisiasa kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutumia vifo kama mtaji wa kisiasa. |
“..Sisi
kama UTPC tunatoa tamko hilo kwa uchungu na pia chama hicho kisitumie
kifo cha Daudi Mwangosi katika maslahi ya kisiasa kwani hatuko tayari na
swala hilo au zoezi hilo la kujenga mnara kwenye sehemu hiyo kwani
tunapinga vikali ujenzi huo unaotarajiwa kufanywa na chama hicho’Alisema
Mihanji.
|
Alisema
ujenzi wa mnara huo ambao inatarijiwa kufanywa na chama sio kazi yao
kwa ili wanatafuta umaharufu wa kwenye majukwaa na kuwataka waache
wakawaachia wahusika wenyewe jumuhia za waandishi wa habari ambao ndiyo
wenye mamlaka na si vinginevyo.
|
Mihanji
alisema kuwa, Mwangosi hakuwa mwanasiasa bali alikuwa ni mwana taalumu
katika tasnia ya habari “Kwani yeye kufuatia mauaji yake hakuwa katika
harakati za kisiasa bali alikuwa kikazi ambayo ni ya kitaaluma kwahiyo
wenye mamlaka ya ujenzi au kufanyiwa jambo fulani la kihistoria ni
wahusika ambao ni wanataaluma wenyewe na siyo chama cha kisiasa.
|
“UTPC
ndiyo wenye mamlaka ya kufanya suala au zoezi hilo na siyo chama hicho
kwahiyo ni vema swala hilo waakaliacha kama lilivyo kwani sisi ndiyo
wahusika kwahiyo tunajua nini tunataka kufanya juu ya Mwangosi kwahiyo
tamko letu ndiyo hilo kwa chama hicho swala hilo liachwe na tuachiwe
wenyewe”Alisema makamu wa rais huyo.
|
Mwangosi
alikuwa mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Chanel ten Mkoani
Iringa ambaye pia alikuwa ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari
Mkoani humo (Iringa Press Club) ambapo ameuawa mikononi mwa jeshi la
polisi mnamo 2012.
Hata
hivyo hadi sasa bado suala la kifo cha Mwangosi limeendelea kupigwa
dana dana kutokana na kesi yake kutosikilizwa na hakuna mwandishi
aliyeitwa kutoa ushahidi wake juu ya mauwaji hayo .
Mwangosi
hakuuwawa kama mwanachama wa Chadema bali aliuwawa akiwa kazini
kutimiza wajibu wake wa kitaalum ya uandishi hivyo kwa kitendo cha
Chadema kutaka kushirikiana na IPC katika ujenzi huo itakuwa ni
kuvuruga mwenendo wa kesi na kupingana na msimamo wa awali ya IPC ,UTPC
na vyombo vingine kuhusu taarifa za awali ambazo jeshi la polisi
lilianza kutaka kupotosha kuwa eti alikuwa ni mwanachama wa Chadema
jambo ambalo si kweli.
No comments:
Post a Comment