Sunday, August 25, 2013

Yanga yaichapa Ashanti mabao 5-1 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam


Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao la pili la timu hiyo dhidi ya Ashanti, lililofungwa na Simon Msuva katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda mabao 5-1. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)


Beki wa timu ya Ashanti, Khan Usimba, akiondoa mpira miguuni mwa Simon Msuva wa Yanga wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
 Msuva wa Yanga, akipiga mpira mbele ya Emmanuel Kichiba wa Ashanti katika mchezo huo.
Golikipa wa Ashanti, Ibrahim Abdallah, akiruka juu huku akiwa amekabwa na mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Wachezaji wa Yanga, wakishangilia bao la pili la timu hiyo dhidi ya Ashanti, lililofungwa na Simon Msuva katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda mabao 5-1.
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao la 3 la timu hiyo, dhidi ya Ashanti.
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao la 3 la timu hiyo, dhidi ya Ashanti.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la 3 la timu hiyo, dhidi ya Ashanti lililofungwa na Jerryson Tegete (10), katika mchezo huo.
Juma Abdalla wa Yanga na Khan Usimba wakikimbilia mpira uliokuwa mbele yao, wakati wa mchezo huo leo.
Didier Kavumbagu wa Yanga akizuiwa na Tumba Suedi wa Ashanti katika mchezo huo, leo Uwanja wa Taifa jijini.
Didier Kavumbagu wa Yanga akijaribu kumkaba Emmanuel Kichiba wa Ashanti.
Simon Msuva wa Yanga akipiga shuti mbele ya lango la Ashati huku akizuiwa na Tumba Suedi wa timu hiyo.
Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo huo, uwanjani hapo.
Mmoja wa mashabiki wa Yanga akionesha mabao 4 kwa timu yake wakati wa mchezo huo, uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment