Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo kuhusu kuanza wakati wowote zoezi la Serikali, kuwarejesha makwao wakimbizi walioingia nchini.
Baadhi ya waandishi wa habari na Maofisa wa Uhamiaji wakisikiliza habari zilizokuwa zikitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, Dar es Salaam leo, kuhusu kuanza wakati wowote kwa zoezi la Serikali, kuwarejesha makwao wakimbizi walioingia nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akizungumzia kuhusu kuanza wakati wowote kwa zoezi la Serikali la kuwarejesha makwao wakimbizi walioingia nchini.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuanza wakati wowote zoezi la Serikali la kuwarejesha makwao wakimbizi walioingia nchini. Kulia ni Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Operesheni, Simon Sirro.
Waandishi wa habari na Maofisa wa Uhamiaji wakisikiliza habari zilizokuwa zikitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, John Nchimbi, Dar es Salaam leo, kuhusu kuanza wakati wowote kwa zoezi la Serikali, kuwarejesha makwao wakimbizi walioingia nchini.
Na Charity James
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi amepiga chenga kuzungumzia suala la kumpa ulinzi Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe.
Hoja ya Dk. Mwakyembe kutakiwa kupewa ulinzi imepigiwa kelele na watu wengi, wakiwemo viongozi wa dini ambao walidai kuwa kiongozi huyo anapambana na kazi ngumu.
Hivi karibuni waziri Dk. Mwakyembe alitangaza kuwafukuza kazi Maofisa kadhaa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius kwa kile alichodai walishiriki kusaidia wasafirishaji wa dawa za kulevya.
Kutokana na hali hiyo, waandishi wa habari leo, walikuwa na kiu ya kutaka kusikia kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Nchimbi atatoa msimamo gani katika kumwekea ulinzi Dk. Mwakyembe.
Hata hivyo, Dk. Nchimbi alijitokeza mbele yao na kudakiza kwa kusema: "Ninajua wengi mnataka kuniuliza maswali nje ya mada yangu (uhamiaji), hivyo sipo tayari kuyajibu leo, labda nitayaweka kiporo.
"Mimi nilikuwa mwandishi wa habari kama nyie, hivyo nikitoka nje kidogo ya maada yangu ninayotaka kuizungumzia leo, nikijibu tu maswali yenu najua kabisa mtakwepesha suala langu la uhamiaji ambalo ndilo ninalozungumzia hapa leo hii," alisema.
Akizungumzia suala la wahamiaji haramu alisema mpaka sasa ni wahamiaji 10,672 wameshaanza kurudi makwao pamoja na mali zao, kasi ya kuondoka inaendelea.
Alisema pamoja na takwimu hiyo waziri amepewa jukumu na Rais Jakaya Kikwete kuwaondoa wale ambao bado hawajaanza kuondoka mara baada ya kuwaruhusu waondoke kwa hiyali bila kulazimishwa.
"Muda muafaka wa kuanza kulishughurikia suala hilo najua mwenyewe ni siku gani ntaanza kuifanya kazi hiyo ambayo shughuri itaanza ghafra na itatekelezwa kama kasi ya umeme," alisema.
Dk. Nchimbi ametoa wito kwa wahamiaji haramu ambao bado hawajaanza kuondoka, amewataka warudi makwao nchi imedhamilia hivyo haitavumilia kuendelea kuwaona katika nchi hii, wanataka kuona watanjzania wanaishi kwa amani.
Alisema kwa muhamiaji yeyote aliyenakiu ya kuendelea kuishi nchini arudi nchini kwake kufuata uraiya ili aweze kuendelea kuishi.
Aidha nchimbi alisema jumla ya wahamiaji 10,672 kati yao mkoa wa Kagera ni wanyarwanda 60,088, warundi 4000, waganda 269, Mkoa wa Kigoma ni warundi 142, Jamhuri ya kidemocrasia ya kongo (DRC), 8 na Mkoa wa Geita ni Wanyarwanda 126 ambao waliondoka Agosti 18 mwaka huu.
Alifafanua kuwa kati ya hao wahamiaji 14 wamerejea tena nchini Tanjzania, hivyo amewataka viongozi wa vijiji kuacha kushirikiana na wahamiaji haramu ni kosa la kisheria na atakayebainika atafikishwa mahakamani.

No comments:
Post a Comment