Sunday, September 8, 2013

JE WAJUA HII AZAM TV ITAKUWA IKITUMIA KAMERA 8 UWANJANI


Kamera za Azam TV zikiwa kazini katika mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC na Ashanti
 Ligi kuu ya mpira wa miguu Tanzania bara wakati wowote itaanza kurushwa moja kwa moja (live) kupitia kituo cha Televisheni cha Azam (Azam TV).

Azam itarusha ligi hiyo katika muonekano mardadi hautakua na tofauti na ule wa ulaya, kwani kamera nane za Azam TV zitatumika kurekodi kila pambano litakalo chezwa.

Kuwepo kwa kamera nane uwanjani, huu ni wastani wa juu wa idadi ya kamera zinazopaswa kuonyesha kwa ufasaha pambano lolote la soka ingawa katika mechi za ligi nyingine au michuano mingine kunakuwa na kamera zaidi za kuonyesha mbwembwe mbalimbali.
Kamera za Azam TV zikiwa kazini katika mchezo wa kirafiki kati ya Azam FC na Ashanti
 Azam TV walitumia mchezo wa kirafik kati ya Azam Academy na Ashanti United uliochezwa katika uwanja wa Azam uliopo ndani ya Complex ya Azam, FC uliochezwa september tano siku ya Alhamisi kujaribia vifaa vyao vitakavyo kuwa vinatumika kurusha matangazo ya moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment