*Nia kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
limetenga maeneo 34 kwa ajili ya uwekezaji katika huduma za malazi kwa wageni
wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi mwa nchi kwa ajili ya utalii.
Maeneo haya ya uwekezaji ambayo
yatahusisha ujenzi wa loji na kambi za kudumu za wageni yatawezesha kuongezeka
kwa vitanda 1,790 vitakavyowezesha kuongezeka kwa uwezo wa shirika kuhudumia
watalii wanaotembelea Hifadhi za Taifa katika kipindi cha miaka mitano ijayo.Maeneo haya 34 yaliyotengwa mahsusi kwa ajili ya kupanua wigo wa huduma za malazi katika hifadhi, yanapatikana katika Hifadhi za Kilimanjaro; Katavi; Mikumi; Mkomazi; Ruaha; Saadani; Tarangire; Rubondo na Kitulo. Kipaumbele kwenye uwekezaji huu umewekwa kwenye Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi, ambazo zina uhaba mkubwa wa malazi na kusababisha idadi ndogo ya watalii.
Uamuzi huu wa TANAPA wa kutenga
maeneo mapya ya uwekezaji umezingatia ukuaji wa sekta ya utalii nchini ambapo
karibu asilimia 75 ya wageni wanaofika nchini kwa ajili ya utalii hutembelea
Hifadhi za Taifa. Hata hivyo, pamoja na idadi ya watalii kuongezeka, idadi ya
watalii wengi hutembelea Hifadhi za Kaskazini tu, wakati Hifadhi za Kusini na
Magharibi zina vivutio vya kipekee na vya ubora wa aina yake.
Hivi sasa idadi ya vitanda katika
maeneo ya hifadhi kwa ujumla inafikia vitanda 6,681 na kwa ongezeko hili katika
kipindi cha miaka mitano ijayo idadi hii itafikia vitanda 8,421.
Katika kuhakikisha kuwa maeneo
haya yaliyotengwa yanapata wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi, jitihada
mbalimbali zitafanywa ili kuyatangaza maeneo haya ikiwa ni pamoja na kuandaa
Kongamano Maalum litakalotangaza fursa za uwekezaji katika hifadhi
linalotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwakani. Kongamano hilo linatarajiwa kushirikisha wawekezaji mbalimbali wakubwa na wadogo kutoka ndani na nje ya nchi ambapo watapata fursa ya kuyafahamu kwa undani maeneo hayo na namna gani uwekezaji wao utakavyoleta faida kwa sekta ya utalii na uchumi wa nchi yetu.
Aidha, shirika limejipanga kwa
maana ya kuandaa miundombinu bora kama vile barabara, madaraja na viwanja vya
ndege ambavyo vitarahisisha zoezi la uwekezaji kwenye maeneo hayo.
Uamuzi wa TANAPA wa kutenga
maeneo haya ya uwekezaji unafuatia jitihada nzuri ambazo zimekuwa zikifanywa na
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja
na Serikali yake za kuvutia wawekezaji nchini pamoja na watalii ambao wataweza
kuongeza pato la taifa.Katika siku za hivi karibuni Tanzania imetajwa kuongoza kwa kuwa nchi inayoongoza kwa kuwa na vivutio bora Afrika ikiyaacha mbali mataifa mengine kama vile Afrika ya Kusini; Botswana na Kenya.
Taarifa hii inatokana na utafiti ulioendeshwa na mtandao wa safaribookings.com wa nchini Uholanzi ambao ni maarufu kwa uchambuzi wa maeneo bora ya utalii duniani.Katika matokeo ya uchambuzi huo Tanzania iliweza kuwa na vivutio kumi (10) kati ya hamsini (50) vilivyo bora kabisa barani Afrika ambapo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ilikuwa ya kwanza kabisa miongoni mwa vivutio hivyo. Hivyo hii imetoa fursa ya pekee kwa wawekezaji kuwekeza kwenye maeneo haya hasa, Ruaha, Mahale, Katavi na Hifadhi zote kwa ujumla.
Vivutio vingine vilivyoifanya Tanzania kuongoza ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Ruaha, Mahale, Gombe, Katavi, Tarangire, Ziwa Manyara na Arusha. Vingine ni pamoja na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Pori la Akiba la Selous.
Ni dhahiri kuwa katika siku za karibuni Tanzania itaweza kuongeza idadi ya watalii kutokana na taarifa hizi na hivyo kuzifanya taasisi kama TANAPA kuanzanza mikakati ya kuongeza idadi ya vitanda katika maeneo ya hifadhi kwa ajili ya kukidhi ongezeko hili.
Imetolewa na Mkurugenzi Mkuu
Hifadhi za Taifa Tanzania
Hifadhi za milima Udzungwa inapatikana katika mkoa wa Morogoro ni moja ya vivutio vinavyopatikana nchini Tanzania.
Hifadhi ya Serengeti ni moja kati ya maajabu Saba Barani Afrika.
Hifadhi ya Mikumi inapatikana Mkoa wa Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akielezea kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mapema hii leo juu ya mikakati ya kuinua utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga maeneo 34 ya uwekezaji, kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
Baadhi
ya waandish wa Habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakati akielezea mikakati ya
kuinua utalii hifadhi za kusini na magharibi kwa kutenga maeneo 34 ya
uwekezaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar
es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maeneo 34 waliyoyatenga
kwa uwekezaji kwa ajili ya huduma za malazi kwa wageni wanaotembelea
Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi kwa ajili ya utalii. Kushoto ni
Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maeneo 34 waliyoyatenga kwa uwekezaji kwa ajili ya huduma za malazi kwa wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi kwa ajili ya utalii. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maeneo 34 waliyoyatenga kwa uwekezaji kwa ajili ya huduma za malazi kwa wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi kwa ajili ya utalii. Wa pili kulia ni Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maeneo 34 waliyoyatenga kwa uwekezaji kwa ajili ya huduma za malazi kwa wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi kwa ajili ya utalii. Wa pili kulia ni Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete.
Wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya Habari, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maeneo 34 waliyoyatenga kwa uwekezaji kwa ajili ya huduma za malazi kwa wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi kwa ajili ya utalii. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maeneo 34 waliyoyatenga kwa uwekezaji kwa ajili ya huduma za malazi kwa wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi kwa ajili ya utalii. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa TANAPA, Pascal Shelutete na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Zamaradi Kawawa.
Baadhi ya waandishi wa habari, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu maeneo 34 waliyoyatenga kwa uwekezaji kwa ajili ya huduma za malazi kwa wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi kwa ajili ya utalii.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za
Taifa (TANAPA), Allan Kijazi, akijibu maswali ya waandishi wa habari
alipokuwa akizungumzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo,
kuhusu maeneo 34, waliyoyatenga kwa uwekezaji kwa ajili ya huduma za
malazi kwa wageni wanaotembelea Hifadhi za Kusini na Magharibi ya nchi
kwa ajili ya utalii. (Picha zote na Eliphace Marwa, MAELEZO na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
No comments:
Post a Comment