Monday, November 11, 2013

UWEZO-TWAWEZA LAENDESHA UPIMAJI WA KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU (KKK) MANISPAA YA SINGIDA


Uwezonineno la Kiswahili lenyemaanaya ‘kipawa au umahiri’. Uwezo ni mradi wa miaka minne wenyelengo la kuboresha ujuzi katika kusoma na kuhesabu miongoni mwa watoto wenye umri wamiaka 6-16 nchini Kenya, Tanzania na Uganda, wakutumia njiabunifu kwenye kuleta mabadiliko ya kijamii ambayo yanatokana na raia wenyewe na kuwajibika kwa umma.
Kwa mwaka huu zoezi la upimaji limeanza hivikaribuni .Hapa kunabaadhi ya picha za matukio ya zoezi la upimaji manispaa ya Singida.
Faiza Ramadhani, mwanafunzi wa darasa lasita, shule ya Msingi Misufini, Manispaa ya Singida, akifanya jaribio la kusoma kamasehemu ya zoezi la upimaji wa stadi KKK. Wanaomuongoza ni Winfrida Makelele (kushoto) na Samwel Msihi (kulia) kutoka shirika la Uwezo.
 Mkazi wa mtaawa Mitunduruni, ManispaayaSingida, Mwanahamis Ali Sembo (kushoto) akitoa maelezo ya kaya yakekwaHadra Mohamed, mkusanyataarifawashirika la Uwezo.
 Hadija Ramadhani, mwanafunzi wa Darasa la Nne, Shule ya Msingi Mitunduruni, ManispaayaSingida akifanya jaribio la kupima stadiza KKK linaloendeshwa na shirika la Uwezo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Kindai, Bw. Athman Masudi Maganga (kushoto) akisikiliza maelezo juu ya matumizi ya dodoso la upimaji wa stadiza KKK, kutoka kwa Mratibuwa Uwezo Wilaya (Manispaa ya Singida), Bibi ZuhuraKayra (kati). Aliyeupande wa kuliani Bi. Shamim Hatibu, mkusanya taarifa wa Uwezo, Mtaa wa Kindai, Singida Manispaa.

No comments:

Post a Comment