Wednesday, January 1, 2014

AJALI YA MKE NA MUME ,MKE APOTEZA MAISHA PAPO HAPO NA DEREVA KUTOKOMEA KIZANI JIJINI DAR ES SALAAM.

Si jambo la kufurahia na si kila kitu kinapangwa na Mungu  blog hii mwaka huu 2014 imeanza na habari ya kusikitisha  ambapo bibi na bwana ,asubuhi   ya leo  01/01/2014 majira ya 12 asubuhi , wakiwa kwenye safari yao huku wakitembea kwa miguu katika barabara ya Mwai Kibaki eneo la Drive  gari aina ya Nadia  iliyotambulika kwa namba za usajili T 104 ATA Ikiwa na Rangi ya Silva  iliacha njia na kuwagonga wapiti njia hao wawili ambao kwa majina hayakutambulika  kwa haraka.

Katika ajali hiyo bibi au mwanamke alipoteza maisha papo hapo huku babu /mme wake akiwa katika hali mbaya ,blog hii iliwasiliana na kituo cha polisi Osterbay na baada ya muda si mrefu Trafiki  mmoja alifika na kisha kuomba msaada kwa raia mwema ambaye alipakia mwili wa  marehemu pamoja na majeruhi ,wakati tukio hilo  la kuwa pakia ndipo napo diffenda ya polisi ilipofika ikiwa  na askari kanzu .

Mashuhuda wa ajali hiyo wanasema tukio hilo limetokea ghafla  na mara baada ya ajali hiyo  ambayo dereva wa gari aina ya NADIA T 104 ATA alizidiwa na gari na kuhama njia kutoka kushoto hadi upande wa kulia na kuwagonga  watu hao waliokuwa wakitembea kwa miguu na kusababisha kifo cha bibi huyo hapo hapo.

Baada ya raia kusuburi kwa muda bila polsi kufika walianza kufunga barabara lakini askari wa binafsi kutoka Kampuni ya WARRIOR SECURITY LTD waliweza kusimamia zoezi la kuongoza magari hivyo kuwezesha magari kuendelea na safari japo madereva tax na boda boda walifunga bara bara kwa kutumia mawe pamoja na viti ya mbao.

Hadi blogger wa blog hii inaondoka eneo la tukio msamaria mwema mmoja  alikuwa ametoa msaada wa kubeba mwili wa marehemu na mwili wa majeruhi kwa kutumia gari lake.

chini ni picha za tukio  la ajali hiyo   pole kwani picha zinasikitisha.
 kulia ni Mwili wa bibi mara baada ya kupata ajali na kufariki papo hapo kushoto ni mwili babu/ mwanaume ambaye alikuwa mahututi  mara baada ya ajali ya mbaya  iliyotokea  leo asubuhi.
 picha hii  wahusika wa ajali wakiwa wamelala  chini huku raia wakiwa wanasubiri msaada kutoka polisi.
Bara bara ikiwa imefungwa kwa mawe na viti vya mbao kwa shinikizo la kuwaharakisha polisi kufika eneo la tukio  ili kumsaidia majeruhi wa ajali hiyo.
 gari la msamaria mwema ambalo limesaidia kubeba mwili wa marehemu na  pia kumpeleka majeruhi Hospitali.MBELE YA GARI NI MASUPERVISOR WA WARRIOR SECURITY LTD ,SPV OMARY MAIRA & OLAIS LEVAVAYO wakiendelea kusimamia zoezi la kuongoza magari
askari wa usalama wa barabarani akisimamia zoezi la kupakia mwili wa marehemu na majeruhi tayari kuwapeleka hospitali
 huyu ndio majeruhi mwanaume akiwa tayari amepakiwa kwenye gari la msamaria mwema tayari kupelekwa hospital
 wasamaria wema wakiwa wamebeba mwili  wa marehemu tayari kupeleka  hospital
 mwili wa marehemu ukiwekwa vizuri kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea hospital
 Askari polisi wakiwasili kwenye eneo la tukio la ajali wakati huo askari wa usalama barabarani alishafika kwenye tukio na kutoa msaada wa kupakia mwili marehemu na majeruhi tayari kuwapeleka hospitali.
 Kushoto ni askari wa WARRIOR SECURITY LTD  akiendelea kuangalia zoezi la magari kupishana wakati wa ajali hiyo mbaya ni supervisor OMARI MAIRA mwenye shati la kaki na suruali nyeusi
hakika hujafa hujaumbika

Mungu ailaze mahali pema peponi Roho ya marehemu bibi na Mungu amponyeshe  babu /majeruhi wa ajali  hakika unajua unapokwenda na hujui tuendako


kama unatarifa zaidi kuhusu marehemu  au majeruhi au  umeliona gari hilo tafadhali toa taarifa mara moja kwa kituo cha polisi kichopo karibu yako au piga namba hizi  za askari wa usalama barabarani  AFANDE  JUMANNE kwa  usaidizi zaidi  0767 479 388

kumbuka gari ni aina ya Nadia rangi ya Silva namba za usajili T 104 ATA.


No comments:

Post a Comment