MAELFU
ya abiria na mamia ya magari yakiwemo mabasi
yanayosafirisha abiria kwenda kanda ya ziwa, yamekwama katika barabara
kuu inayounganisha mikoa ya Dodoma na Morogoro, katika eneo la Dumila,
wilayani Kilosa baada ya daraja kuu la Dumila kukatika kutokana na
mvua kubwa ilionyesha wilayani Kilosa usiku
wa kuamkia Januari leo.
Kuvunjika kwa daraja hilo kumesababishwa na mafuriko makubwa na hivyo kusababisha
nyumba na watu kukosa makazi kutokana na
mvua hiyo inayodaiwa kunyesha maeneo ya milimani wilayani Kilosa.
Mafuriko hayo pia yamesababisha kusombwa kwa nguzo za umeme,
miti mikubwa kukatika na kutanda
barabarani huku shule ya sekondari ya wasichana Dakawa, chuo cha Veta Dakawa
mahakama ya mwanzo Dakawa nazo kuathirika.
Watu wanadaiwa kufa maji huku wengine walionekana wakiwa
juu ya miti kusubiri kuokolewa.
Kwa mujibu wa wenyeji wa eneo hilo mafuriko hayo yalianza
majira ya saa 12 asubuhi na kwamba
mafuriko hayo hayajawahi kutokea kwa
zaidi ya miaka 15 sasa ambapo mvua kama hiyo ilitokea 1995.
Mpaka sasa hakuna huduma
zozote za kijamii, na bidhaa zilizopo eneo hilo, vitu kama chakula na maji, vimekuwa bei juu na kusababish adha kubwa
kwa abiria hao.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera alifika eneo la
Tukio kujionea hali halisi, na amewataka
wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali inafanya utaratibu wa kuwaokoa walioko
juu ya miti na kutoa misaada kwa walioathirika zaidi.
Alisema kuwa kutokana na hali mbaya hiyo ya mafuriko
serikali ya mkoa imelezimika kuomba helikopta kwa ajili ya kuokolea wananchi hao
ambao wengine wamekwama katika mabati ya nyumba zao.
|
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akimsikiliza Meneja wa Tanroad Bi Doroth Mtennga |
|
Wananchi wakiwa wamehifadhi mizigo juu ya mapaa ili kuiokoa na madhara ya mafuriko |
|
Maelezo zaidi kutoka kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi |
|
Wananchi wakipeana msaada katika kujiokoa kutoka katika mkondo wa maji |
|
Hii ni shule ya Msingi Magole, ikiwa imezungukwa na maji, hali inayomaanisha shughuli za elimi pia zimesimama |
|
Wananchi kutoka katika kijiji cha Magole wakivuka kuelekea Morogoro |
Shughuli ya kuvuka ikiendelea...
Kila mbinu ilitumika kuhakikisha kwamba mwisho wa siku kila mtu anavuka salama
Hawa walikwama juu ya paa
No comments:
Post a Comment