Siku
ya terehe 1 ya mwezi wa pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni
KUANZIA SAA TATU NA NUSU ,kutakuwepo na mkutano mkubwa wa wanamasumbwi
wote ulioitishwa na orgnaizesheni ya ngumiza kulipwa Tanzania (TPBO) kwa
lengo la kuwakutanisha mapromota wote,mabondia na makocha wa ngumi
wote kwa lengo la kujadili ngumi za kulipwa zinapoelekewa,kujuana na
kuelimishana sheria za ngumi za kulipwa zinavyotumika kinyume na sasa
,sheria nyingi zinafungiwa macho na kutumia uzoefu zaidi kuendesha mgumi
nchini. Mkutano huo ulioitishwa na Rais wa TPBO bw Yasin Abdallah
akishirikiana na Ibrahim kamwe na Mapromota wa ngumi chini ya ufadhili
wa kitwe Traders unatarajiwa kuwa mkutano wa kwanza kuwakutanisha
mapromota wote pamoja na mabondia wa ngumi za kulipwa wa hapa nchini
ili kuboresha ngumi na kuhamasisha wadhamini na makampuni wajitokeze
kuudhamini mchezo huo ,ambao ndio mchezo unaoliletea mataji na sifa
Tanzania katika medani za kimataifa lakini hauna udhamini wowote ,mpaka
sasa ni mchezo ambao unaojiendesha wenyewe kwa nguvu za wadau
wachache wachovu na mabondia wenyewe ambao uwezo wao ni mdogo sana
kukikidhi matakwa kamili ya mchezo wenyewekam ilivyo kwa wenzetu,ni
mchezo ambao una huduma nyingi zinazohitaji nguvu ya wadhamini
ili uendelee kuboreka zaidi.
Akizungumza
na vyombo vya habari katibu wa ngumi za kulipwa nchini bw Ibrahim kamwe
, amesema imewaalika viongozi wa baraza la michezo (BMT), na viongozi
wengine wote wa ngumi za kulipwa watakuwepo kama vile Emmanuel
mlundwa,names kavishe, makaranga,Onesmo ngowi,kinyogoli, matumla,
Zuwena kibena(mama zugo) na viongozi wadau wa karibu na ngumi wamealikwa
kuhudhulia mkutano huo ambao utafanyika Siku ya terehe moja ya mwezi wa
pili katika ukumbi wa vijana hall kinondoni. hivyo kamwe alimaliza kwa
kuwaomba kila anaejijua kuwa yeye ni bondia wa ngumi za kulipwa na
promota wangumi ahudhurie bila kukosa mkutano huu muhimu sana kwa
wamasumbwi ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment