Thursday, January 30, 2014

MABOMU YAFURUMUSHWA KWENYE MSIBA WA ALIYEKUWA SHEIKH WA MKOANI MARA KUWAZUIA WAFUASI WA CHADEMA WASIMFANYIE FUJO MBUNGE WA ZAMANI WA MUSOMA MJINI CCM

NA. Mwandishi wetu
Musoma.
POLISI mkoani Mara wamelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wafuasi wanaotajwa kuwa niwa Chama cha maendeleo na demokrasia nchini CHADEMA waliokuwa wakimfanyia fujo aliyekuwa mbunge wa zamani wa Musoma mjini Bw. Vedastus Manyinyi Mathayo wa CCM.
Mathayo ambaye pia alikuwa mjumbe wa NEC inatajwa kuwa amefanyiwa vurugu hizo leo wakati alipokuwa akishiriki kuhani msiba wa aliyekuwa Sheikhe wa Musoma  Othman Magee aliyefariki dunia juzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alipelekwa kwaajili ya kupatiwa matibabu mara baada ya kuhamishiwa toka hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza ambapo ilishindikana.
Taarifa zinasema kuwa mara baada ya Mkutano wa hadhara wa CHADEMA kumalizika wanachama wa chama hicho wakiwa wameambatana na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Wilbrod Slaa pamoja na mbunge wa Musoma mjini Mhe. Vicent Nyerere walielekea kwenye msiba kwaajili ya kujumuika na wafiwa na wananchi wengine.
Wanachama hao walipofika kwenye msiba huo na kumkuta mbunge wa zamani Musoma mjini Bw. Mathayo walianza kumshambulia kwa maneno na katimaye mawe huku wengine wakiburuta pikipiki zao na kulifanya eneo hilo kuwa na hali tete hata baadhi ya magari yakipondwa mawe kwenye eneo la msiba huo.
Dakika chache baadaye polisi walifika katika eneo la msiba ambalo lilikuwa si tulivu tena na kujaribu kuituliza hali kwa njia za kidiplomasia na iliposhindikana walilazimika kurusha mabomu ya machozi ili kupata kuwatawanya wafuasi hao.
Marehemu Sheikh Othman anatarajiwa kuzikwa kesho mjini Musoma.

Taarifa zaidi kuwajia:- ITAENDELEA
 
habari kwa hisani ya g Sengo blog

No comments:

Post a Comment