Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
(katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi wa
shirikisho la waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam,waliomtembelea
ofisini kwake leo.Mh. Lowassa alikutana na viongozi hao kupanga
utaratibu wa kufanya harambee ya kuchangia saccos ya shirikisho
hilo.Mwezi Disemba mwaka jana,Mh Lowassa alikuwa mgeni rasmi katika
tamasha la bodaboda kwenye viwanja vya leaders jijini Dar es Salaam
ambapo aliahidi kukutana na uongozi huo kwa ajili ya kuandaa harambee ya
kuwasaidia kumiliki pikipiki waendesha bodaboda wa Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment