Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb)
amesisitiza umuhimu wa Tanzania kuridhia uraia wa nchi mbili ili
Watanzania wanaoishi ughaibuni waweze kufaidika na fursa za kiuchumi na
kijamii zinazotolewa kwa raia katika nchi wanazoishi.
Mhe.
Waziri alitoa kauli hiyo katika ufunguzi wa kongamano lililoandaliwa na
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) na kufanyika katika Hoteli ya JB
Belmont jijini Dar es Salaam tarehe 22 Januari, 2014.
Kongamano
hilo ambalo linawakutanisha wawakilishi kutoka Serikalini, wanazuoni,
asasi za kiraia na watafiti mashuhuri lina lengo la kujadili njia
mbalimbali ambazo wanadiaspora wanaweza kuzitumia kuchangia maendeleo ya
nchi yao kwa mazingira ya Tanzania.
Mhe.
Waziri aliwambia wajumbe wa kongamano hilo kuwa hoja ya uraia wa nchi
mbili itawasilishwa na kutetewa katika Kikao Maalum cha Bunge la Katiba
ambacho kinatarajiwa kufanyika katika siku za karibuni.
“Endapo
uraia wa nchi mbili utaridhiwa, Watanzania wanaoishi ughaibuni wataweza
kupata kazi nzuri na kukopa benki katika nchi wanazoishi, hivyo kipato
chao kitaongezeka ambacho watakitumia pia kuwekeza nyumbani. Mhe.
Waziri alisikika akisema.
Mhe.
Membe alitolea mfano wa nchi zilizoweka mazingira mazuri ya
wanadiaspora katika kuchangia maendeleo ya nchi zao kuwa ni pamoja na
Nigeria, Ghana na Kenya.
Awali,
akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo, Mkuu wa Shirika la
Kimataifa la Uhamiaji hapa nchini Bw. Damien Thuriaux alisema kuwa,
kongamano hilo ambalo litafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 29 Januari 2014
lina lenga kuhamasisha uratibu wa masuala ya Uhamiaji na Diapora kwa
kuzishirikisha Wizara na Taasisi mbalimbali.
Aidha
katika kushirikiana na Serikali ya Tanzania, Bw. Damien alisema kuwa
Shirika lake litasaidia uundwaji wa Tovuti maalum kwa ajili ya watu
waishio Nje (Diaspora) na masuala mengine yanayohusu uhamiaji.
No comments:
Post a Comment