Saturday, February 15, 2014

DALA DALA LA KONDAKTA MKATISHA BARABARA (ROUTE)NA MNYANYASAJI WA ABIRIA

Picha ni dala dala linalofanya safari zake katika barabara ya kawawa kutoka Ubungo kwenda Masaki na kurudi tena Ubungo namba zake za usajili ni T 419 AAH Aina  ya coster na mbele inamaandishi ya COSTER mbele ya kioo cha dereve .

daladala hilo kwa nyuma 
picha zote na Gasper sambweti (www.sambweti.blogspot.com)
 Kondakta wa daladala hii anasifika kwa lugha za kivita na matisho kwa abiria wote waonao panda daladala hiyo  kutoka Masdki kwenda Ubungo au Ubungo kwenda Masaki.

Jana blog hii ilishuhudia  unyanyasaji kwa abiria unafanya na kondakta wa daladala hiyo aliyekuwa amevalia tishet nyekundu yenye maandishi ya SIMBA kwa nyuma kinyume kabisa  na taratibu za mamlaka ya usafirishaji.

Sakata la unyanyasaji lilianza maeneo ya  Darajani karibu na white Inn baada ya kondkta wa daladala moja la Masaki Ubungo kuwafaulisha  abiria wanne wenye jinsia ya kike ili waweze kufikisha Ubungo kondakta huyo mnyanyasaji alikubali na kupewa pesa yaani nauli ya abiria hao wanne .


Safari ilianza na baada ya hatua chache alianza kudai pesa kwa abiria wale tena kana kwamba hakulipwa pesa zao ,watatu kati ya abiria hao walipofika eneo la kituo cha lion walishuka na kondakta kushindwa nguvu kwa kuwa walikuwa wasichana watatu matata.

Safari ilindelea na daladala ilipofikia kituo cha kijiweni dada mmoja ambaye alikuwa amevalia tishet nyekundu na jinzi bluu aliomba kushuka na ndipo hapo  kero ilipoanza baada ya kudaiwa  alipe nauli angali  kondakta laishalipwa na kondakta mwenzake kabla ya kuwapakia  kutoka kituo cha Darajani .


Hali likuwa mbaya hadi dada yule alipoamua kutoa tikiti ya daladala lile alilokuwa amepanda hapo awali lakini kondakta yule  aligoma na  kuamua kukataa kumshusha dada yule mpaka atakapo mlipa tena  nauli ingali alishalipwa na kondakta mwenzake.

Kondakta kwa kujiamini aliamuaru gari kuondokta na dada yule kuendelea kubaki kwenye daladala wakati alipaswa kushushwa katika kituo cha Kijiweni,dada yule alipoona kama masihara alimua kutoa pesa ila ashushwe lakini  kondakta alikuwa mkali pale alipodiwa tikiti na dada yule  hivyo gari liliendelea na safari na lilipofika eneo moja kabla ya kufika kituo cha Shekilango dala dala hilo liliamua kuchepuka na kuacha njia kuu na kupita njia za panya huku kondakta akitoa lugha chafu kwa abiria  bila kujua amebeba kina nani kwenye daladala na bila kujua kuwa gari hilo lina leseni  sio kwa sababu ya kutembea tu barabarani bali kutoa huduma stahili kwa wananchi ambao sasa kondakta ameanza kuwanyanyasa na kuwanyima haki yao ya msingi ya kushuka katika vituo husika .


Dala dala hilo lilikatisha na kupitia njia za panya mwisho tulitokea katika daraja la  barabra ya SAMNUJOMA na kondakta kuamuru abiria wote washuke kwani ndio mwisho wa daladala na kugoma kufika Ubungo ,



Angali katika daladala hilo kulikuwa na wazee na wakinamama wenye watoto wadogo na wengine wakionekana kuwa wageni kabisa wa eneo lile kwa kifupi walikuwa wamepotezwa kwa kufikishwa eneo wasilolijua .

Kwa kuepusha vurumai abiria wote tulishuka huku wengine tukihofia  usalama wa mali zetu kutokana na usalama wa eneo tulikoachwa na dala dala kisha dala dala hilo kutokomea kuelekea eneo la Oil com karibu na Ubungo Mataa .

Nilijikongoja kwa miguu hofu ikiwa imetanda yapaya majira ya saa tatu za usiku kutoka eneo hilo la bondeni lenye gereji ya magari mabovu na kila aina ya vitisho  na nilistaajabu kufika mbele eneo la  kituo cha mafuta cha Oil com na kukuta dala dala ile imesimama na inapaikia abiria wanaokwenda BUGURUNI .

Nilisiomama na kupiga picha hizi chini kwa ungalifu mkubwa na bila kutumia mwanga ili kuepuka kadhaa ya kondakta mnyanyasaji na kumbuka dada yule nae alishushwa kule bondeni kwa nguvu  angali alaitakiwa kushushwa  kituo cha sinza kijiweni .

SWALI LINAKUJA JE DALADALA HIZI ZIPO KWA AJILI YA KUSAIDIA WANANCHI AU ZIPO BARABARANI ILI KUNYANYASA WANANCHI ?


WAPI MAMLAKA HUSIKA

 hizo ndizo namba za usajili za dala dala hilo

 DALA DALA LILIPO KATIKAT NA PEMBENI MWENYE TISHET NYEKUNDU NI KONDKTA WA DALA DALA HILO
picha zote na Gasper sambweti (www.sambweti.blogspot.com)
       DALA DALA LILIPO KATIKATA NA PEMBENI NI KONDKTA WA DALA DALA HILO picha zote na Gasper sambweti (www.sambweti.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment