Tuesday, February 25, 2014

KAMPUNI YA ASTARC YAZINDUA SHOWROOM MPYA YA KUUZA PIKIPIKI TANZANIA

Baadhi ya wananchi wakipata maelekezo kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Astarc Group wakati wa uzinduzi wa aina mpya ya Pikipiki ijulikanayo kwa jina la Hero Dawn leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Eliphace Marwa - Maelezo)
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa aina mpya ya Pikipiki ijulikanayo kwa jina la Hero Dawn Bw. Subhash Patel (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Pikipiki hizo zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Astarc Group leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Astarc Group Bw.Salil Musale na kulia ni Mkurugenzi wa Astarc Group Africa Bw. Sameer Musale.
Subhash Patel ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Pikipiki mpya aina ya Hero Dawn akijaribu moja ya pikipiki aina ya Hero Karizma inayotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya Astarc Group
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa aina mpya ya Pikipiki ijulikanayo kwa jina la Hero Dawn Bw. Subhash Patel (kushoto) akiteta jambo na Afisa Uhusiano wa kampuni ya Astarc Group Bw. Mukesh Joshi  leo jijini Dar es Salaam. kulia ni Mkurugenzi wa Astarc Group Africa Bw. Sameer Musale
Mkurugenzi wa Astarc Group Africa Bw. Sameer Musale akitoa historia fupi ya kampuni ya Astarc ambayo ni watengenezaji na wasambazajiwa pikipiki aina ya Hero ambazo zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni ya Astarc Group akimkaribisha mgeni rasmi Bw, Subhash Patel (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa aina mpya ya pikipiki ijulikanayo kwa jina la Hero Dawn.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa aina mpya ya pikipiki Hero Dawn  Bw. Subhash Patel akizungumza na waaandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa aina mpya ya pikipiki ijulikanayo kwa jina la Hero Dawn(Pesa zaidi mfukoni) mapema leo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Astarc Group Bw.Salil Musale akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa aina mpya ya pikipiki ijulikanayo kwa jina la Hero Dawn (Pesa zaidi mfukoni) mapema leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wakijibu maswali mbalimbali kuhusu pikipiki aina ya Hero Dawn wakati wa uzinduzi wa pikipiki hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi, Subhash Patel pamoja na uongozi wa kampuni hiyo, wakifurahia uzinduzi huo.


Dar es Salaam Tanzania, 25.02.2014 
KAMPUNI ya Astarc Motors Tanzania leo hii inayo furaha kubwa kuwafahamisha watanzania wote kwamba imefungua rasmi showroom yake mpya na kubwa ya kuuza pikipiki aina ya HERO-Dawn iliyopo barabara ya Pugu mkabala na kiwanda cha sigara jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa halfa fupi ya ufunguzi wa show room hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Astarc Motors Tanzania ltd Bw. Sameer Musale  alieleza kuwa miongoni mwa aina hiyo ya pikipiki pia kampuni hiyo ina aina nyingine kama vile Splendor NXG, Glamour, Hunk and Karizma zenye ukubwa wa kuanzia cc 100 hadi cc 225.
"Hili ni tukio la kihistoria kwa pikipiki za miguu miwili Tanzania kwa uzinduzi wa show room hii kubwa ya kuuza pikipiki aina ya HERO Dawn, katika kukidhi mahitaji ya wateja wetu wa Tanzania ambapo pikipiki hii ilitengenezwa kwa ajili yao na kila kitu kilifanyiwa hapa Tanzania" alisema Sameer.
Aliongeza kwamba spea za pikipiki hizo aina ya HERO Dawn zinapatikana hapa hapaTanzania kwa bei nafuu sana na wamba kila mteja ataweza kuzinunua na kampuni hiyo tayari imekwishazileta spea hizo kwa wingi zenye kuweza kukidhi mahitaji kwa miezi 6 kuaznia leo hii.

Akifafanua Mkurugenzi huyo alisema kua kutokana na majairbio ya miezi 6 Tanzania kwa madereva wa bodaboda pikipiki hii ya HERO Dawn inaweza kusafiri  kwa mwendo kusafiri umbali wa kilomita 65 kwa kutumia lita 1 ya mafuta na unaweza kubadili spea zake mara chache sana tofauti na zingine na hivyo kuweza kutumia gharama kidogo sana kuihudumia.
Mwisho kampuni hiyo imelenga kuhakikisha usalama, umakini na ubora kwa madereva na abiria wake na pia ina uhakika wa kukonga nyoyo ya watanzania wote kwa bidhaa hiyo.
Historia ya kampuni hiyo:

Makao makuu ya kampuni hiyo yapo India na pia ni wauzaji wakubwa wa pikipiki ulimwenguni pote ambapo inauza pikipiki milioni 6 kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni jumla ya pikipiki milioni 50 zilizouzwa ulimwenguni kote tangu mwaka 1985.

No comments:

Post a Comment