Monday, February 24, 2014

Milioni 50 za Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ kutolewa Ijumaa


Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania Ijumaa hii itachezesha droo kubwa ya promosheni yake ya 'Mimi Ni Bingwa' ambayo itamfanya mmoja wa wateja wake kujishindia zawadi ya kitita cha shilingi milioni 50.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde alisema droo hiyo itakayobadilisha maisha ya mtu, imepangwa kuchezeshwa katika ofisi za makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

"Baada ya miezi kadhaa iliyojaa zawadi kwa wateja wetu waaminifu, Ijumaa hii itakuwa ndiyo kilele cha promosheni yetu ya Mimi Ni Bingwa ambapo tutamtafuta na kumtangaza mshindi wa zawadi yetu kubwa," alisema.

Jane alisema kuwa mshindi atakayebahatika atapatikana kwa kuchezesha droo ya bahati na sibu utakaokuwa chini ya uangalizi na usimamizi wa afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania na kushuhudiwa na wafanyakazi wa Airtel na vyombo vya habari.

"Ningependa kuwashukuru wateje wetu kwa kushiriki promosheni hii na kuwakumbusha wateja wote wa Airtel ambao bado hawajajiunga na mchezo huu kwamba bado wanaweza kujiunga na wanaweza wakawa na bahati ya kushinda zawadi kubwa ya shilingi milioni 50 kwa sababu wote waliojisajili katika promosheni wataingizwa katika droo hii kubwa na ni namba moja tu itakayobahatika. Hii ina maana kuwa kadri uchezavyo ndipo unapata nafasi kubwa ya kuibuka mshindi,” alisema.

Alisema kuwa wakati wa promosheni, wateja wa Airtel walijishindia pesa taslim ya zaidi ya shilingi milioni 324 na zaidi ya tiketi 36 kwa ajili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda kuangalia mechi ya klabu ya Manchester United katika uwanja wa Old Trafford zilitolewa.

"Promosheni ya Airtel ‘Mimi Ni Bingwa' imeweza kubadilisha maisha ya wateja wake kwa kuwazawadia zaidi ya shilingi milioni 324 pesa taslim na kuwapa watanzania 36 nafasi ya kipekee katika maisha yao ya kuitembelea klabu kubwa ya soka ulimwenguni ya Manchester United pamoja na kuitembelea uwanja wao wa Old Trafford na pia kuwa sehemu ya mashabiki wa soka wanao angalia mechi ya Manchester United moja kwa moja ‘live’ uwanjani," alisema.

“Kwa mara nyingine tena, hii ni nafasi kwa wateja wengine wa Airtel ambao hawakujisajili kwenye promosheni kuingia kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wenye neno “BINGWA” kwenda namba 15656, na kujibu maswali mengi iwezekanavyo, unaweza jishindia zawadi kubwa ya pesa taslim ya shilingi milioni 50,” alisema.

Promosheni ya Airtel ‘Mimi ni Bingwa’ iliyoanza mwezi Novemba mwaka jana, ni matokeo ya ushirika baina ya klabu ya Manchester United na kampuni hii ya mawasiliano, ambayo hailengi tu kuwazawadia wateja wake pekee lakini pia kuwaunganisha washiriki wa promosheni hii na soka la kimataifa ambapo itasaidia kuamsha ari ya michezi miongoni mwa watanzania, hasa katika soka.

Wakati wa promosheni hiyo, washindi wawili wa Mimi Ni Bingwa walijishindia zawadi ya shilingi milioni moja kila moja kwa kila siku, washindi wawili walijishindia zawadi ya shilingi milioni 5 kila mmoja kila wiki na mshiriki mmoja alikuwa anajishindia tiketi mbili kila wiki kwa ajili ya safari iliyogharamiwa kila kitu ya kwenda Old Trafford.

Kundi la awamu ya kwanza la washindi wa tiketi tayari walifurahia safari yao na imebainisha kuwa kundi la pili na la tatu watasafiri kwenda Manchester ifikapo mwezi Machi wakati Manchester United ikitarajiwa kucheza tena katika uwanja wake wa Old Trafford.

No comments:

Post a Comment