Sunday, February 2, 2014

NGASA AIFIKISHA TENA YANGA KILELENI, YAIFUNGA MBEYA CITY 1-0 LEO



Mshambuliaji wa Yanga ya Dar es Salaam Mrisho Khalfan Ngassa leo amefanikiwa kuipatia timu yake ya kwanza pointi 3 muhimu baada ya bao lake pekee kuizamisha timu ngumu ya jiji la Mbeya, Mbeya City ndani ya uwanja wa taifa.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa imevunja ugumu wa kutokufungwa hata mcezo mmoja kwa timu hiyo ya  Mbeya ambayo imekuwa ikifanya vyema na kuzikamia timu zote za ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Kwa matokeo hayo sasa yanga imerudi kileleleni kwa kufikisha pointi 35 ikifuatiwa na Azam FC iliyo na Pointi 33 na Mbeya City ikibaki nafasi ya 3 na pointi 31 huku Simba ikiwa nafasi ya nne kwa pointi 30 lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi.























































































No comments:

Post a Comment