Tuesday, February 11, 2014

WAFANYABIASHARA MWANZA KUGOMA TENA LEO...??



Mmoja kati vipeperushi vya ujumbe ambavyo vilikuwa vikisambazwa leo na wafanyabiashara katika mitaa ya Uhuru Dampo, jijini Mwanza ili kupata uungwaji mkono wa hatua ya mgomo.
PICHA NA PETER ISUTI.
Ujumbe huu ambao haijajulikana umeandaliwa na akina nani kutokana na kukosa anuani unasomeka hivi :-NDUGU MFANYABIASHARA MKOA WA MWANZA UNATAKIWA KUFUNGA BIASHARA YAKO KUANZIA SASA NA KWA MUDA USIOJULIKANA ILI KUUNGANA NA WENZETU NCHI NZIMA AMBAO TAYARI WAMEKWISHA ANZA MGOMO HADI HAPO MHESHIMIWA RAIS ATAKAPO TOA TAMKO JUU YA MADAI NA MALALAMIKO YA WAFANYABIASHARA NCHINI.

Awali wafanyabiashara wa maduka muhimu ya mitaa ya katikati ya jiji la Mwanza waligoma kwa takribani siku tatu na kuwapa wakati mgumu wananchi walio taabika kupata huduma muhimu hata hivyo waliamua kurejea wenyewe shughulini wakishuhudia wakipata hasara kubwa huku tarehe za kulipa kodi zikifika na wakitakiwa kulipa kodi za mapango ya biashara wanayoyatumia.

Swali lina baki pale pale, Jeh Wafanyabiashara wa Mwanza watagoma tena?

No comments:

Post a Comment