*Wawataka wananchi wa Chalinze wamchague Ridhwani Kikwete
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mdogo wa
Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete, akiwa katika Mkutano na
Wazee wa Kimasai walipokuwa wakijadilina juu ya suala la Wafugaji wa
Chalinze na Pwani kwa Ujumla,jana Machi 17,2014 kwenye Ukumbi wa
Masai,Chalinze
Mbunge
wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka akiwaomba Wananchi wa
Lugoba, Jimbo la Chalinze kutofanya makosa kwenye Uchaguzi Mdogo ndani
ya Jimbo lao na Wampigie Kura, Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete. Sendeka
aliyasema hayo jana Machi 17,2014 katika Mkutano wa Kampeni uliofanyika
kwenye Uwanja wa Sokoni wakati alipopita kuwasalimia WanaChalinze
Mbunge wa Jimbo la Longido, Lekule Laiza akiwasalimia Wana Chalinze.
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya Kadi mbili za
Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi wa
Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi ni
Kassim Msakamali (hayupo pichani)
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akiwainua mikono Wanachama
wapya wa Chama cha Mapinduzi,Kassim Msakamali (wa pili kushoto)
na Mrisho Issa (wa pili kulia) ambao wote ni Wananchi wa Kijiji cha
Msata, Chalinze.Kulia ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la
Chalinze (CCM), Steven Kazidi.
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,
Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza machache wakati
alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji
cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete aiwasalimia wananchi wa Lugoba, Chalinze.
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa amekabidhiwa fimbo ikiwa ni
ishara ya kusimikwa na kuwa Laigwanani wa Kimasai na Laigwanan Ole
Masingijana . (Picha zote na Othman Michuzi)
No comments:
Post a Comment