WAZIRI
MKUU Mizengo Pinda ameagiza huduma za upimaji wa figo zitolewe kwa
kuzunguka katika kanda zilipo nchini na kuacha utamaduni wa kutoa huduma
hizo wakati wa maadhimisho hayo tuu.
Alisema hayo Jana mchana (Alhamisi,
Machi 13, 2014), wakati wa akifunga kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya
Afya ya Figo Duniania yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere mkoani
Dodoma, yenye kauli mbiu Figo Huzeeka kama wewe. Jali Afya ya Figo zako.
Akizungumza
na wananchi wakati wa kilele hicho Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi
kujenga utamaduni wa kujali na kupima afya zao mara kwa mara: ‘‘Tumieni
fursa hii ya uwepo wa huduma hizi karibu nanyi kujua hali ya afya ya
figo zenu ili mchukue hatua stahiki mapema, kuchelewa kujua afya yako
kunaweza kuathiri pia urahisi wa matibabu kama ukigundulika kwamba
umeathirika na Ugonjwa wa Figo“.
Alisema, huduma kama hizi za Klinic ya Umma yaani Public Clinic
zitolewe mara kwa mara kikanda bila kusubiria maadhimisho ili kuweza
kuwafikia wananchi kwa wakati na kuendelea kuhamasisha huduma za afya za
aina hii kwa wananchi, walau kuweza kutoa huduma hizi katika Kanda ya
juu Kusini, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi na Kanda ya Kaskazini
mtakuwa mmefanya jambo la busara sana kwa watanzania.
Waziri Pinda alisema,
zipo njia muhimu za kuzingatia ili kuepukana na ugonjwa wa figo kama
inavyoelezwa na wataalum kuwa ni pamoja na kufanya mazoezi kwa wingi,
kunywa maji glass 6 hadi 8 kila siku, kuacha kuvuta sigara, kuzingatia
uzito wa mwili na kuacha kutumia dawa kabla ya maelekezo ya daktari,
aliongezea Waziri Pinda.
Waziri Mkuu alisema,
‘‘Dawa hapa ni Kinga na Sio Tiba“ hivyo aliwaomba wananchi kujenga
utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuweza kufahamu na
kupunguza madhara makubwa ya ugonjwa huu.
Changamoto kubwa iliyopo
mbele yetu kama serikali ni upungufu wa madaktari bingwa wa kutosha wa
kutibu magonjwa ya figo, kupandikiza figo na gharama kubwa za matibabu
ya figo ambayo huduma hiyo haipatikani hapa nchi hivyo: ‘‘Serikali
itachukua jukumu la kuongeza idadi ya wataalamu wa figo na kwa
kuzingatia suala hili tutaliweka katika bajeti ya Serikali ya mwaka“,
alisema Waziri Mkuu.
Alieendelea kusema kuwa,
kuna Sera ya Magonjwa ya Afya ya mwaka 2007,Miongozo na Mikakati ya
kupambana na ugonjwa huu hivyo, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa
kushirikiana na Taasisi ya Taifa ya Figo Tanzania, itazindua ripoti ya
Wiki ya Afya ya Figo 2013 Tanzania, ambapo ripoti hiyo itaonesha kuwa
watu 4,325 walijitokeza kupima afya za figo zao na kati ya hao asilimia
15 (623/325) walipatikana na matatizo ya figo. Ni dhahiri kuwa, juhudi
hizi za kubaini ukubwa wa tatizo la ugonjwa wa Figo, zinazofanywa na
Serikali zitarahisisha na kuwezesha wananchi wengi kupata taarifa
mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi kuhusu afya ya figo.
Pamoja na kuhudhuria
Kilele cha maadhimisho hayo, Waziri Mkuu alizindua rasmi tovuti ya
Taasisi ya Taifa ya Figo ambayo itakuwa inalezea masuala yote yanayohusu
figo na kusisitiza wananchi kutumia tovuti hiyo kujifunza masuala yote
masuala mbalimbali ya figo.
Mapema,
Prof. Ephata Kaaya, ambaye ni Mjumbe wa Bodi Taasisi ya Taifa ya Figo
alieleza kuwa dira na malengo ya taasisi hiyo ni kuwa kitovu cha taifa
katika kuendeleza na kuthibiti magonjwa ya figo kwa kuendelea kutoa
elimu kwa wingi, kufanya tafiti mbalimbali ili kuweza kufaham takwimu
halisi za ugonjwa huo, kwani katika maadhimisho haya jumla ya wananchi
3800 wameweza kusajiliwa na wananchi 3120 wamefanyiwa uchunguzi.
Taasisi
ya Taifa ya Figo itaendelea kushirikiana na Wizara ya Afya, Sekta
Binafsi na wananchi kuendesha masuala ya matibabu ya figo na kubuni
mbinu mbadala ya upatikanaji wa fedha ili kuweza kuendesha Taasisi hiyo
ambayo hivi sasa inatoa huduma za matibabu ya figo katika Hospitali ya
Taifa Muhimbili, Hospitali ya Rufaa Mbeya, na huduma hizo pia
zitaanzishwa katika Hospitali za Rufaa Bugando na KCMC.
No comments:
Post a Comment