Saturday, March 15, 2014

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAKATIBU WA BUNGE MAALUM LA KATIBA DODOMA



Rais Jakaya Kiwete leo Machi 14, 2014 asubuhi amewaapisha Makatibu Wakuu wa Bunge Maalum la Katiba katika halfa iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Kilimani mjini Dodoma. Walioapishwa leo ni Katibu Mkuu wa Bunge hilo Yahaya Hamisi Hamad na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Thomas Kashilila.



Rais Jakaya Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bunge Maalum la Katiba Ikulu ya Kilimani Dodoma leo baada ya kuwaapisha Makatibu wa Bunge hilo. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Yahaya Hamisi Hamad, Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta, Makamu Mwenyekiti, Samia Suluhu Hassan na Naibu Katibu Mkuu, Dk. Thoas Kashilila.



Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Makutibu wapya wa Bunge maalum la Katiba mara baada ya kuwaapisha Ikulu ya Kilimani Dodoma jana. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Bunge hilo, Yahaya Hamisi Hamadi na kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Dk. Thomas Kashilila.

No comments:

Post a Comment