Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Vifaa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael katika hafla iliyofanyika leo Wizara ya Biashara ZanzibarKatibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian Raphael kulia akitoa neno la Shukran baada ya Makabidhiano ya Gari na Vifaa kwa Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula. Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Sungula kulia akimkabidhi Funguo ya Gari Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian Raphael,kushoto ni Elizabeth Lukaza Mchambuzi wa Shirika la UNDP Tanzania.Hafla imefanyika leo Wizara ya Biashara Zanzibar.(Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar)
Na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar,
WIZARA
ya Biashara na Viwanda ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekabidhi
Gari na Vifaa vya Ofisini kwa Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko ya
Zanzibar katika hafla iliyofanyika leo Wizarani Malindi mjini Unguja. Msaada
huo uliofadhiliwa na Shirika la Biashara la Dunia WTO ulitolewa ili
kuijengea uwezo Wizara ya Biashara ya Zanzibar katika kukabiliana na
majukumu yake ya kila siku. Akikabidhi
Msaada huo Mkurugenzi Sera na Mipango wa Wizara ya Biashara ya Bara
Edward Sungula kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara ya Zanzibar Julian
Raphael amesema Suala la Biashara ya Kimataifa ni la Muungano hivyo
Serikali mbili lazima zishirikiane na kusaidiana katika kutekeleza
majukumu yao. Amesema
Msaada huo ni utekelezaji wa Mradi wa “Capacity Building for Trade
Development and Integration Project” ambao una lengo la kuzijengea uwezo
Serikali katika kutekeleza misaada chini ya utaratibu wa “AID FOR
TRADE”.
Ameongeza
kuwa msaada huo ni mwanzo wa kudumisha ushirikiano katika kutekeleza
mradi huo na njia ya kuendeleza kudumisha Muungano uliopo baina ya
Tanzania Bara na Zanzibar. Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Masoko Zanzibar Julian
Raphael ameishukuru Wizara hiyo juu ya Msaada huo na kuongeza kuwa
utachochea ufanisi katika majukumu yao. Katika
kutekeleza Mradi huo wa kukuza Sekta ya Biashara Tanzania Bara na
Zanzibar Mradi umeanza kwa kununua Vifaa ambavyo ni pamoja na Gari
mbili, Komputa, Projekta na Mashine ya Kuchapishia.
No comments:
Post a Comment