Sunday, May 4, 2014

Bondia Myweather amshinda kwa pointi Maidana

*Mabondia maarufu wa Tanzania washuhudia mpambano huo kwenye luninga live Igo Lounge Sinza jijini Dar es Salaam 


Marcos Maidana punches as Floyd Mayweather Jr. defends during their fight at MGM Grand.
Bondia Floyd Myweather (kushoto), akipangua ngumi ya Marcos Maidana wakati wa mpambano wao uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo.
Floyd Mayweather Jr. punches Marcos Maidana during their fight at MGM Grand.
Bondia Floyd Myweather (kushoto), akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Marcos Maidana wakati wa mpambano wao uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo.
Mabondia wa Tanzania Karama Nyilawila (kushoto), Rashidi Matumla na Fransic Cheka wakifuatilia kwa makini mpambano huo uliochezwa alfajiri ya leo katika ukumbi wa Igo Lounge, Sinza Mapambano jijini Dar es Salaam, walipokuwa wakionesha live kupitia luninga kubwa kwa mashabiki wa mchezo huo. (Picha zote za Dar es Salaam na Super D, Mnyamwezi)
Marcos Maidana defends against Floyd Mayweather Jr. during their fight at MGM Grand.
Bondia Floyd Myweather (kushoto) akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Marcos Maidana wakati wa mpambano wao uliochezwa alfajiri ya kuamkia leo. Myweather ameshinda kwa Point za majaji, Judge Michael Pernick scored it 114-114, a draw. Bert Clements had it 117-111 and Dave Moretti score it 116-112 


Hili lilikuwa ni tangazo la mpambano huo lililokuwa likitokea kwenye luninga kabla ya mpambano huo.
Mabondia Rashid Matumla (kushoto), Fransic Cheka na Karama Nyilawila, wakifuatilia mpambano wa Myweather na Maidana kupitia luninga katika ukumbi wa  Igo lounge, Sinza Mapambano jijini Dar es Salaam leo pamoja na wadau mbalimbali wa masumbwi nchini.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT), Anderson Lukelo, mabondia Rashid Matumla (kushoto), Francis Cheka na Kalama Nyilawila, wakifuatilia mpambano wa Myweather na Maidana kupitia luninga katika ukumbi wa Igo lounge, Sinza Mapambano jijini Dar es Salaam leo pamoja na wadau mbalimbali wa masumbwi nchini.
Mashabiki wa ngumi wakifurahia mchezo wa ngumi kupitia luninga.
Myweather na Maidana wakichapana live kwenye luninga leo alfajiri.
Bondia Fransic Cheka akitoa tathmini ya mchezo ulivyokuwa baada ya Myweather kutangazwa mshindi
Bondia Karama Nyilawila akitoa tathmini ya mchezo ulivyokuwa baada ya Myweather kutangazwa mshindi
Wadau mbalimbali wakipiga picha na Cheka
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA mbalimbali wa Tanzania, alfajiri ya kuamkia leo wamejitokeza kuangalia mpambano uliokuwa ukifanyika Marekani kati ya bondia Floyd Myweather na Marcos Maidana, mpambano uliokuwa ukifanyika  katika ukumbi mkubwa kabisa wa ngumi duniani MGM grand.

Nchini Tanzania mpambano huo, ulishuhudiwa na mabondia maarufu kama vile Rashidi Matumla, Karama Nyilawila pamoja na Fransic Cheka pia Makamu wa Rais Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini (BFT), Anderson Lukelo pamoja na kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'. 

Wadau hao wa ngumi, walijumuika kwa pamoja kuangalia mpambano huo live katika ukumbi wa Igo lounge, Sinza Mapambano.


Mpambano huo, ambao ulikuwa mkali na kushuhudiwa dunia nzima na wapenda mchezo huo.

Hata hivyo mpaka dakika ya mwisho ya mpambano huo, ulimalizika kwa bondia Floyd Myweather kushinda kwa pointi za majaji wawili na mmoja wa majaji akitoa droo. 

Majaji Michael Pernick salitoa poniti 114-114, Bert Clements 117-111 na Dave Moretti akatoa 116-112.

Wakizungumzia mpambano huo, bondia Rashid Matumla alisema kuwa wenzetu wana uwezo mkubwa sana katika masumbwi hata katika kujaji Maidana alikuwa anacheza fujo tu katika mchezo huu hivyo ndio kitu kilicho mnyima ushindi.

Naye Cheka aliongeza kwa kusema siku zote bingwa analindwa sana hivyo myweather ameweza kutetea taji lake vizuri

Bondia Kalama amesema mambo haya yanatokea kila siku mana nakumbuka zama za Tyson ndio watu walikuwa wanajazana namna hii kuamka alfajili kuangalia ngumi sasa Myweather anatisha kachukua urithi wa Tyson, huyu bondia ni mzuri kwa kutembea awapo ulingoni kacheza vizuri nimemfurahi. 

No comments:

Post a Comment