Thursday, May 15, 2014

Mfuko wa Wanyamapori yawataka wananchi kushiriki kuwalinda wanyamapori


 Kaimu mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Bw. John Muya akitoa wito kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kushiriki katika mapambano dhidi ya ujangili ili kulinda rasilimali za Taifa ambazo ziko hatarini Kutoweka. Kulia kwake ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Georgina Misama,kutoka  kushoto  ni  Afisa Habari wa Mfuko huo Bi. Tabu Nziku, Kaimu Katibu Tawala wa Mfuko huo Bi Antonia Raphael. (Picha zote na Frank Mvungi, Maelezo)

Kaimu mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Bw. John Muya akiwaeleza waandishi wa habari mafanikio yaliyofikiwa  na Mfuko  huo katika Kupambana na Ujangili katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.




Na Georgina Misama-MAELEZO
MFUKO wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (TWPF) umebuni miradi ya maendeleo kama vyanzo vya mapato ili kukabiliana na changamoto ya ufinyu wa bajeti katika kutekeleza majukumu yake.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa mfuko huo Bw John Muya wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Alisema kwamba mfuko umebuni miradi ya maendeleo ili kujiendeleza kwa kuongeza mapato ambapo alitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa Jengo la Kakakuona na Pori la akiba la Pande.

Miradi mingine ni Bustani ya Wanyamapori ya Tabora, Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila-Songea na kambi ya Utalii katika Pori la akiba Selous.

Muya alisema TWPF husimamia ukusanyaji wa maduhuli, usimamizi wa uwindaji wa kitalii na wa wenyeji, utalii wa picha, biashara ya wanyamapori hai na mazao yatokanayo na wanyamapori, mashamba na bustani za ufugaji wa wanyamapori.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa TWPF Bi. Antonia Raphael alisema mfuko hugharamia shughuli mbalimbali za  usimamizi wa wanyamapori ikiwa ni pamoja na usimamizi wa maeneo ya jumuia za hifadhi za wanyamapori (WMAs), kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii na uendelezaji wa miundombinu katika mapori ya akiba.

Mfuko  hufanya malipo ya kifuta machozi kwa wananchi ambao ndugu zao wameuawa au kujeruhiwa na wanyamapori ambapo kwa kipindi cha miezi mitatu Januari –Machi 2014, kiasi cha shilingi milioni 9 kililipwa kwa ajili waliouwawa. 

No comments:

Post a Comment